Ziara ya Waziri wa mambo ya nje wa Burundi Utruki VISA ilikuwa sababu

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlüt Çavuşoğlu akutana na waziri wa mambo ya nje wa Burundi Alain Aime Nyamitwe
Katika ziara yake nchini Uturuki waziri wa mambo ya nje wa Burundi Alain Aime Nyamitwe amekutana na waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevulüt Çavuşoğlu.
Katika mkutano wao viongozi hao walijadili kuhusu ushirikiano baina ya Burundi na Uturuki.
Katika mazungumzo yao walizungumza kuhusu hati za safari kwa wanadiplomasia wa nchi hizo mbili.
Viongozi hao waliafikiana na kusaini mikataba tofauti katika sekta ya kilimo, utamaduni  na sanaa.
Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki  katika mkutanao na waaandishi wa habari  alisema kuwa Uturuki unaunga mkono juhudi katika sekta tofauti  barani Afrika ikiwemo nchini Burundi.
Vile vile alizungumzia kuhusu kikosi cha kulinda amani nchini Somalia na kusema kuwa idadi kubwa ya wanajeshi ni askari kutoka Burundi.
Viongozi hao walizungumzia pia kuhusu kundi la FETÖ ambapo milki za kundi hilo kama shule zitakabidhiwa shirika la Maarif.
Kundi la FETÖ sio tishio kwa Uturuki pekee bali kwa mataifa yote.
Serikali ya Burundi ilichukua hatuo ya kufunga shule hizo na kuzikabidhi shirika la Maarif. ripot ya TRT
Uturuki itashirikiana na Burundi kutatua matatizo yanayoikabili .

0 Comments:

Post a Comment