TAARIFA KWA UMMA
15 JUNI 2017
MIAKA MINNE TOKA TUKIO MAUAJI YA SOWETO ARUSHA
NI tukio lisiloweza kusahaulika katika mioyo na akili za watu wa Arusha na Watanzania kwa ujumla. Maisha ya wapendwa wetu yalipotea katika tukio la mauaji yaliyokuwa na sura ya kupangwa kimkakati. Hatuwezi kusahau.Familia za wapendwa waliopoteza ndugu zao, Kamanda wetu Mama Judith William Moshi na Mtoto Fahad Jamal, Mungu aendelee kuwapa uvumulivu wa maumivu mliyopitia na ujasiri Familia, WanaCHADEMA na Watanzania kwa ujumla. Tukio hili limeacha vilema wengi ambao mpaka leo baadhi yao wapo kwenye matibabu na kuwa na maisha tegemezi.
NI miaka minne lakini bado maswali kuhusu mauaji haya hayajajibika. Serikali imeonyesha udhaifu mkubwa hasa kwa kushindwa kuonyesha wivu na maisha ya wananchi wake. Ufuatiliaji wa tukio hili la kutisha ndio kama hakuna tena. Ukweli hauzami, iko siku ukweli utadhihirika na kuna watu wataaibika.
Dhamira mbaya na ovu ililengwa kwa viongpzi wakuu wa chama akiwemo Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Mhe Freeman Mbowe, alikuwepo Mbunge waArusha Mjini Mhe Godbless, Viongozi wa Kanda ya Kaskazini, Mkoa wa Arusha na Wilaya ya Arusha Mjini na Madiwani wa Jiji la Arusha.
Serikali hii ya awamu ya TANO kwa mwenendo wake, ndio inatupa mashaka zaidi. Nafasi ya serikali katika kutimiza wajibu wake kwenye ulinzi na usalama wa raia, imekuwa ni nadharia ya maneno, lakini hamna kitu. Japo kwenye hili moja, tunaitaka serikali ijikaze na kueleza alipo Ben Saanane apatikane akiwa hai. Serikali ya CCM ijue kuwa, mwisho umekaribia sana tena umeshafika Watanzania hawatamuuliza tena Ben Saanane, kitafuata kilio na kilio hicho tutalia wote. Bora Mungu atuepushie mbali kwa sababu wanaodhani hawatalia kumbe wao ndio watalia sana.
Kwenye kumbukumbu hii ya miaka MINNE, tuikumbushe serikali ya CCM kuwa, Watu wasiposema kwa maneno, watasema kwa matendo na matendo ya mtu aliyezuiliwa kusema kwa maneno akiamua kusema kwa matendo hawezi kuzuiliwa kutenda. Ndani ya miezi michache ijayo serikali ya CCM isiporuhusu haki ya kikatiba kwa vyama vya siasa kufanya mikutano ya kisiasa na kutangua kauli batili ya kuzuia mikutano ya hadhara ya kisiasa na kuondoa tishio la watu kukutana kwa uhuru, kuna uwezekano wa Watanzania kuanza kusema kwa matendo.
Aidha kwenye kumbukumbu hii ya miaka MINNE, CHADEMA Kanda ya Kaskazini hatukubaliani na kauli za serikali ya CCM kuhusu kutamka wazi wazi kuwa itawashughulikia watu mathalani wabunge wakiwa nje ya BUnge. Hii sio kauli ya hekima, sambamba na kauli nyngine zenye kuwapa Wakuu wa MIkoa na Wilaya nguvu na jeuri inayowafanya kutumia mamlaka yao vibaya. Huku kushughulikiana kutawafanya wananchi kujiandaa kupambana na wanaoshughulika.
CHADEMA Kanda ya Kaskazini, kwa Mkuu wa Mkoa au Wilaya atakayetumia mamlaka yake vibaya tutashughulika nae, hatutakubali uovu utawale na tutawaambia wananchi washughulike nao bila woga. Na tunamuomba Mhe RAIS awe msikivu sana kwenye mambo ya msingi tutakayomletea kuhusu mambo ya hovyo hovyo ambayo hawa watelue wake watakuwa na wamekuwa wanayafanya. Tutayafanya kwa nia njema na mapenzi mema ya Taifa hili.
Mungu Ibariki Tanzania – Mungu Ibariki CHADEMA
Imetolewa LEO tarehe
15 Juni 2017
Amani Golugwa
KATIBU WA CHADEMA – Kanda ya Kaskazini
0 Comments:
Post a Comment