CHADEMA YARIDHIA AGIZO LA SERIKALI LA KUHAMISHA SHUGHULI YA MAZISHI KUTOKA SHUJAA HADI MAJENGO

TAARIFA CHADEMA KANDA YA KASKAZINI 03.06.2017

Taarifa rasmi kuhusu MABADILIKO YA UWANJA TAREHE 5 JUNI

Mwili wa aliyekuwa Mbunge mstaafu na Muasisi wa CHADEMA Mhe.Dr. Phillemon Ndesamburo sasa utaagwa (state funeral) Juni 5 katika uwanja wa Majengo uliopo Moshi Mjini. Siku hiyo itakuwa ni fursa kwa wakazi wa Moshi na Tanzania kwa ujumla kufanya kumbukizi ya maisha ya Mzee Ndesamburo mwasisi wa siasa za mageuzi nchini.

Tukio hilo Maalumu la kumbukizi la maisha ya Marehemu Dr.Phillemon Ndesamburo litaanza katika viwanja hivyo saa 3 asubuhi na mwili utawasili uwanjani hapo saa 5 asubuhi. Viongozi wakuu wa Chama wakiongozwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Mhe.Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dr. Vincent Mashinji watashiriki tukio hilo sambamba na Wajumbe wa Kamati Kuu, Wabunge, Viongozi wa Dini na wawakilishi wa Serikali.

Aidha siku hiyo wananchi wote watapata fursa ya kuaga na kutoa heshima za mwisho.

Imetolewa na;
Mozec Joseph
Afisa Habari CHADEMA Kanda ya Kaskazini

0 Comments:

Post a Comment