Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amesema wizara yake inafuatilia kwa karibu kubaini watekaji na watu wanaokamata na kuchukuliwa watu wengine nchini.
Kauli hiyo aliitoa mjini Dodoma wakati wa mahojiano na vyombo vya habari nje ya Ukumbi wa Bunge baada ya wabunge kuitaka serikali itoe tamko kutokana vitendo ya utekaji na kuchukuliwa watu kuendelea kujitokeza nchini.
Waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba |
“Tayari wizara yangu inashughulikia suala hilo la kutekwa msanii Roma Mkatoliki na kuchunguza ili kuona ni nani anahusika katika utekaji huo, kwani anaweza kuwa asiwe askari na mtu mwingine akatumia mavazi ya askari kufanya utekaji huo,” alieleza Mwigulu.
Mwigulu alisema kama serikali kupitia wizara yake inatakiwa kufanya mambo kwa uhakika pamoja na kuchunguza ndipo itoe taarifa kuhusu jambo lolote.
Alisema tayari wizara yake imechukua hatua za kuchunguza jambo hilo la msaniii Roma.
Ndani ya Bunge wakati wakichangia Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, wabunge waliuliza kwanini serikali inanyamaza kimya kutoa tamko wakati wimbi la kutekwa watu na kukamatwa na kupotea bila kueleweka wapo wapi linaendelea kutokea nchini.
0 Comments:
Post a Comment