Waziri wa mambo ya ndani wa Uturuki Suleyman Soylu amesema, shambulizi lililotokea kwenye jengo la polisi mkoani Diyarbakir, kusini mashariki mwa Uturuki ni la kigaidi.
Akizungumza kwenye mahojiano na chombo binafsi cha habari Haberturk, Soylu amesema mlipuko huo ulisababishwa na mabomu yaliyowekwa kwenye barabara ya chini ya ardhi. Katika mlipuko huo, askari polisi mmoja na raia wawili waliuawa.
Watuhumiwa watano walikamatwa mapema leo ikiwa ni sehemu ya uchunguzi wa shambulizi hilo
0 Comments:
Post a Comment