China Kushirikiana na Marekani kiuchumi ,Majeshi

Rais wa China Xi Jiping kushoto na Rais wa Marekani Donald Trump

Rais Xi Jinping wa China na rais Donald Trump wa Marekani wamezungumza kwa njia ya simu leo asubuhi.
Rais Xi amesema ziara aliyofanya hivi karibuni nchini Marekani imepata mafanikio makubwa na anatarajia kuwa nchi hizo mbili zitatumia ipasavyo mazungumzo manne ya ngazi ya juu kati yao ilikusukuma mbele utekelezaji wa mpango wa siku 100 kuhusu ushirikiano wa kiuchumi, kupanua mawasiliano na ushirikiano kwenye mambo ya majeshi, utekelezaji sheria, mtandao na utamaduni. Pia kuimarisha mawasiliano na uratibu katika masuala makubwa ya kimataifa na kikanda, kuhimiza maendeleo mapya ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili, na kufanya juhudi kwa pamoja ili kusukuma mbele amani na maendeleo ya dunia.
Rais Trump amesema nchi hizo mbili zintakiwa kupanua ushirikiano katika pande zote, na kwamba anatarajia kufanya ziara ya kiserikali nchini China.
Marais hao pia wamebadilishana maoni kuhusu masuala ya peninsula ya Korea na Syria.

0 Comments:

Post a Comment