SimbaChawene: "Rais Huyu anahimiza uwajibikaji , anaondoa Rushwa"

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene amesifu utendaji uliotukuka wa Rais, Dk John Magufuli huku akimtia moyo kuwa, kamwe asisikilize kelele za wanaojaribu kutaka kumvunja moyo, akisisitiza yeye si wa kwanza, kwani hayo yapo tangu serikali ya awamu ya kwanza.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene.
Alisema tangu awamu iliyoongozwa na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na waliomfuatia, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete, walilalamikiwa, lakini wapotoka madarakani walionekana mashujaa na kupongezwa.
Aliyasema hayo bungeni juzi jioni wakati akihitimisha hoja ya mjadala wa bajeti ya wizara yake aliyoiwasilisha Jumanne wiki hii na kujadiliwa kwa siku tatu, sambamba na bajeti ya wizara nyingine ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambayo pia ipo katika Ofisi ya Rais.
“Enzi za Nyerere, walitolea wapinzani, waasi leo hii Nyerere bado anaheshima, akaja Rais Mwinyi alionekana anaendesha mambo kiholela baada ya kufungua uchumi huria, wakapatikana wa kulaumu, lakini kipindi hicho kikapita, amekuja Mkapa akaleta nidhamu ndani ya serikali, katika utumishi serikalini, akaambiwa ameleta ugumu wa maisha, akalaumiwa sana, kipindi hicho kikapita na tunakikumbuka na tunakipongeza sana.
“Amekuja Kikwete, Rais mpole, mjuzi wa diplomasia, ameijenga nchi yetu kujulikana sana kimataifa, amejenga uchumi na miundombinu, amefanya mambo makubwa, akaambiwa ni rais dhaifu, tena ni mpole aliyepitiliza na bahati nzuri waliosema wengine wapo humu…leo anapongezwa sana,” Aliongeza kuwa, utawala wa Magufuli haujapoteza mwelekeo, bali unasonga mbele kwa kasi, akitolea mfano ya hivi karibuni ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), katika ripoti yake ya ukuaji wa uchumi, imeonesha Tanzania ni ya pili Afrika ikiwa na ukuaji wa asilimia 7.1.
Itanguliwa na Ivory Coast pekee ambayo uchumi wake inakuwa kwa asilimia 7.6. “Katika sifa hii ya kupongezwa hata na IMF na jumuiya nyingine za kimataifa. Watu wanajifanya hawaioni. Rais huyu anahimiza uwajibikaji,anaondoa rushwa… watu hawaoni,” alisema

0 Comments:

Post a Comment