Korea Kaskazini imeionya Marekani kutoanzisha vitendo vya uchokozi katika eneo la Korea ikisema kuwa iko tayari kulipiza kisasi kupitia mshambulio ya kinyuklia.
Taifa hilo limesema hivyo wakati ambapo kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un, amehudhuria gwaride la heshima katika mji mkuu wa Pyong yang, akiadhimisha siku ya kuzaliwa ya babu yake, marehemu Kim II-Sung, ambaye ni mwanzilishi wa taifa hilo.
"tumejiandaa kwa vita kamili'' ,alisema Choe Ryong-hae, anayeaminika kuwa mu wa pili mwenye uwezo mkubwa katika taifa hilo.
''Tuko tayari kulipiza kisasi na mashambulio ya Nuklia kwa mbinu zetu dhidi ya shambulio lolote la Kinyuklia''.
Bado nchi hiyo inaendelea na maonesho ya silaha .
0 Comments:
Post a Comment