MAPENDEKEZO ya kuwa na Mamlaka ya Mji Mdogo wa Haydom mkoani Manyara yamejadiliwa katika vikao vya awali vya Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira, Bunge limeelezwa.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo alitoa taarifa hiyo bungeni alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mbulu Vijijini, Flatei Massay (CCM) aliyetaka kujua ni lini serikali itaupa mji wa Haydom hadhi ya Mamlaka ya Mji Mdogo.
Naibu Waziri Jafo alisema mapendekezo hayo yalijadiliwa katika vikao vya awali vya kamati vilivyofanyika Septemba 25, 2012, Baraza la Madiwani katika kikao cha Oktoba 19, 2012 na Kamati ya Huduma za Uchumi katika kikao cha Juni 13, 2014.
Alisema kimsingi vikao vyote vimekubaliana na wazo la kuanzisha Mamlaka ya Mji Mdogo wa Hydom.
Selemani Jafo |
0 Comments:
Post a Comment