HAWA NI MARAIS WALIOCHAGULIWA WAKIWA NA UMRI MDOGO , KABILA NAYE YUMO


Katiba za nchi mbalimbali zimeweka wazi umri unaofaa kwa mtu kugombea nafasi ya uongozi hasa Rais ingawa kiwango hicho hutofautiana kulingana na nchi; kwa mfano, Tanzania mgombea wa Urais lazima aanzie miaka 40 na kuendelea.
Zipo pia nchi nyingine ambazo kigezo cha umri sio muhimu sana kumfanya mtu agombee nafasi hiyo na wakati mwingine nafasi hiyo hurithiwa…sasa leo April 13 nimekutana na list ya Maraisi waliowahi kuchaguliwa wakiwa na umri mdogo duniani hadi kufikia 2017 ambapo Rais sasa wa Korea Kaskazini Kim Jong Un akiwa ndiye Rais mdogo zaidi kuwahi kuchaguliwa.
1: Kim Jong Un 
Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un anashikilia rekodi ya kuwa Rais mdogo zaidi kuwahi kuchaguliwa duniani ambapo aliingia madarakani akiwa na umri wa miaka 26 mwaka 2011 akirithi kiti cha baba yake Kim Jong Il. Sasa Rais Kim ana umri wa miaka 33.
2: Tamim Bin Hamad 
Ni Rais wa Qatar ambaye aliteuliwa kushika wadhifa huo mwaka 2013 akiwa na umri wa miaka 30. Tamim Bin Hamad ana umri wa miaka 35 kwa sasa akikamata nafasi ya pili kuwa Rais mwenye umri mdogo zaidi duniani.
3: Jigme khesar
Huyu ni Mfalme wa Bhutan, nchi ndogo katika Bara la Asia inayopakana na China na India. Mfalme wa nchi hii ndiye kiongozi mdogo zaidi kuwahi kuteuliwa wakati anaanza uongozi wake. Jigme khesar aliteuliwa kuwa Mfalme wa nchi hiyo akiwa na umri wa miaka 25 mwaka 2006. Sasa ana umri wa miaka 37.
4: Atifete Jahjaga
Atifete Jahjaga anashikilia rekodi ya kuwa Rais mdogo mwanamke kuwahi kuchaguliwa duniani. Jahjaga alikuwa Rais wa Kosovo kuanzia April 2011 akiwa na umri wa miaka 35 na kumaliza muda wake mwaka 2016 akiwa na umri wa miaka 40.
5: Andrzej Sebastian Duda
Andrzej Duda ni Rais wa sita wa Poland ambaye alichaguliwa mwaka 2015 akiwa na umri wa miaka 42. Kabla ya kuwa Rais wa nchini alikuwa Mbunge wa Bunge la Ulaya.
6: Joseph Kabila 
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila alichaguliwa mwaka 2001 siku kumi baada ya kifo cha baba yake Laurent Kabila wakati huo akiwa na umri wa miaka 28. Joseph Kabila ana umri wa miaka 45 kwa sasa.

0 Comments:

Post a Comment