MBOWE AKABIDHI AMBULANCE MBILI JIMBONI KWAKE HAI







image.jpegimage.jpeg


Mbowe akifurahia jambo na mtoto ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja ambaye alimkimbilia mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa mkutano.







image.jpegimage.jpeg
Magari ya wagonjwa yenye namba za usajili T 502 DDL na T 503 DDL pamoja nanmuonelano wake wa ndani.


image.jpeg
Mbowe akizungumza na wananchi kabla ya kukabidhi magari hayo
image.jpeg

Mbowe akimkabidhi gari la wagonjwa mchungaji Kiongozi wa KKKT, Mch Asanterabi Swaiimage.jpeg
Daktari wa Machamr Hospital akipungua wananchi wakati akiondoka na gari walilokabidhiwa
image.jpeg
Bwana Afya wa halmashauri ya wilaya ya Hai, Dr Paul Chawote akipokea funguo za gari la wagonjwa toka kwa mbunge wa Hai, Mbowe.


image.jpegimage.jpeg
Mbowe akiagana na wananchi kwa kupeana mikono mara baada ya kukabidhi magari ya wagonjwa

Mbunge wa jimbo la Hai, Freeman Mbowe ametoa magari mawili ya kubebea wagonjwa (Ambulance) kwa wananchi wa jimbo lake.

Tukio hilo limetokea Leo kwenye mji mdogo wa Bomang'ombe ambapo moja kalitoa  kwa hospital ya wilaya ya hai na Nyingine kwa hospital teule ya Machame ambayo ipo chini ya kanisa la KKKT.

Amesema kuwa amenunua magari hayo toka nchini Japan na yameingia nchini toka oktoba mwaka jana lakini amechelewa kuyakabidhi kutokana na urasimu, hila na giliba za baadhi ya watendaji serikali ambao wamekuwa wakiweka mbele siasa na kusahau wajibu wao wa msingi wa kuwatumikia wananchi.

Alisema kuwa kwa kipindi Cha zaidi ya miezi minne alikuwa anafuatilia kupata msamaha wa kodi kwani yanaenda kutumika kwenye hospital ya halmashauri na hospital ya kanisa Taasisi ambazo zinakidhi kupatiwa msamaha wa kodi lakini serikali ilikataa kwa fikra potofu kuwa yanaenda kumpa sifa Mbowe hivyo amelazimika kuyalipia sh milioni 13.4 kila moja hivyo jumla ameyalipia kodi ya sh milioni 27.

"Niwaombe haya magari yatumike kusaidia wananchi wote tena naomba Mungu mtu wa kwanza kuyatumia awe mwanaCCM ili wale waliokuwa wanayazuia wajue kutofautisha masuala ya Maendeleo na siasa ...

"Wale mtakaopewa dhamana wa kuyaendesha niwaombe muyatunze, msiyatumie kwenda bar kupata supu au nisiyakute pale Kwasadala yanabeba ndizi na nyanya," ameonya Mbowe.

Hata hivyo aliwaasa watendaji wa halmashauri kuhakikisha wanalitunza gari hilo na kuhakikisha linatoa huduma kwa wananchi badala ha kuliegesha kwenye ofisi za halamshauri ambapo aliwaambia kama hawawezi kulihudumia wamweleze ili afanye hivyo kwa garama zake


"Nimewapa magari haya yakiwa mazima kabisa nimeyakatia bima  na mafuta nimewawekea full tank naombeni sana muyatunze," anakazia Mbowe

0 Comments:

Post a Comment