Dr SLAA ZIARANI MAREKANI

KATIBU MKUU DK. WILLIBROD SLAA ZIARANI NCHINI MAREKANI

Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa ameondoka nchini jana (Jumamosi Aprili 11, 2015) kuelekea nchini Marekani ambako atakuwa na ziara ya kikazi ya siku tisa.

Dk. Slaa katika safari hiyo ameambatana na mkewe Josephine Mushumbusi.

Ziara hii ya siku tisa ni mwaliko wa Gavana wa Jimbo la Indiana Mike Pence pamoja na taasisi mbalimbali za nchini humo ikiwemo vyuo vikuu kutokana na kutambua mchango wa kisiasa na kijamii wa Dr Slaa na Chadema katika maendeleo ya bara la Afrika na kipekee nchini Tanzania.

Ziara hiyo itamwezesha Dk. Slaa kushiriki mijadala mbalimbali inayohusu uwekezaji, elimu na uongozi iliyoandaliwa kwa ajili yake ambayo lengo lake kuu ni kuitangaza Tanzania kwa ukamilifu wake.

Kwa malengo hayo, Dk Slaa atafanya mihadhara (Public Lectures) kwenye vyuo vikuu vya Purdue, Indianapolis na Marion. Sanjari na mihadhara hiyo, Dk Slaa atakua na vikao vya mashauriano na baadhi ya Maprofesa waadhiri wa vyuo vikuu mbalimbali kwa lengo la kubadilishana uzoefu juu ya masuala ya kisiasa na maendeleo na kijamii na ushiriki wa Chadema katika siasa za Kimataifa.

Zaidi, ziara hii itamkutanisha pia Katibu Mkuu na viongozi na watendaji wakuu wa kiserikali na makampuni mbalimbali pamoja na taasisi kubwa za uwekezaji kwa lengo la kubadilishana uzoefu katika masuala ya uchumi na uwekezeji Barani Afrika na kwa kipekee Tanzania.

Imetolewa na:
Deogratias Munishi
Mkuu wa Idara ya Mambo ya Nje – CHADEMA

0 Comments:

Post a Comment