MEYA JAFAR AVUNJA UKIMYA UBUNGE WA MOSHI MJINI

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi, Jaffar Michael amefungua pazia kwa wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kutangaza nia ya kugombea Ubunge Moshi mjini.

Meya huyo alikwenda mbali zaidi na kukitaka Chama Cha Mapinduzi (CCM), kujiandaa kisaikolojia kuwa chama cha upinzani, kwani mwaka huu kitaangushwa kama alivyoangushwa Goodluck Jonathan wa Nigeria.

Michael alitoa kauli hiyo mwishoni mwa juma katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Kiusa mjini Moshi. Mkutano huo ulikuwa na lengo la kufafanua masuala mbalimbali ya mji huo wa kitaifa na kimataifa.

Baada ya kumaliza hotuba yake, meya huyo aliruhusu maswali kutoka kwa wananchi na ndipo mkazi mmoja wa eneo hilo alipomuuliza kama atakuwa tayari kugombea ubunge katika Jimbo la Moshi Mjini. Swali hilo liliwafanya wananchi kulipuka kwa makofi na mmoja wao alimtunza aliyeuliza swali hilo kwa Sh10,000.

Akijibu swali hilo, meya huyo alisema kama mbunge wa sasa, Philemon Ndesamburo ataamua kupumzika, yeye atachukua fomu ya kuwania ubunge na atasimama kama chama chake kitampendekeza.

Hata hivyo alisema, hata kama chama chake hakitapendekeza jina lake, atakuwa tayari kumuunga mkono mgombea yeyote atakayepitishwa na upinzani.

Kuhusu CCM kujiandaa kisaikolojia, Michael alisema wapo Watanzania wana shaka kwamba Ukawa inaweza isiingie Ikulu na kusema safari hii lazima ing'oke.

"CCM kianze kujiandaa kisaikolojia, alisema.

mwaka huu lazima king'oke," alisemaa

, mwaka wa mwisho wa CCM kuongoza nchi hii ni mwezi Novemba mwaka huu wa 2015. Mwezi huu Ukawa itaingia Ikulu na kuizaa Tanzania upya,"alisema.

"Kila mmoja ajiandae na CCM wajiandae kisaikolojia kuwa chama cha upinzani katika taifa hili. Watu wengi wanaamini kama vile haiwezekani lakini hata Goliati alipopigwa na Daud hakuamini"

"Daudi na udogo wake na jeshi lake dogo alimpiga Goliati. Kwa hiyo CCM ni Goliati aliyeoza kabisa ambaye tutamuondoa bila yeye mwenyewe kuamini kama Jonathan alivyoondolewa Nigeria,"alisema.

Hatua ya Meya kutangaza nia kunamfanya awe mgombea wa kwanza kutoka Chadema wakati CCM ni Priscus Tarimo, Buni Athman Ramole, Amani Ngowi, Halifa Kiwango,Michael Mwita na 


Source gazeti mwananchi

0 Comments:

Post a Comment