MWENYEKITI wa Taifa wa Baraza la Wanawake Chadema, (BAWACHA),
HalimaMdee, amesema kuwa Muungano wa Wanawake wanaharakati wa
Katibawamewasaliti wanawake nchini kwa tamko lao walilotoa wakidai
kuwa katiba pendekezwa imezigatia maslahi ya wanawake kupata haki zao.
Aidha, amewakaribisha aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Rais
yaMabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu, Joseph Warioba pamoja na
wajumbewenzake ambao ni wanachama wa Chama Cha Mapinduzi, (CCM) ,
kujiungana Chadema endapo tume iliyoundwa na kamati Kuu ya CCM
kuwachunguza
itafikia uamuzi wa kuwafukuza kwenye chama hicho tawala
Mdee aliyasema hayo oktoba 20, mwaka huu wakati akizungumza na umati
mkubwa wawananchi kwenye uwanja wa Getrude Mongela vilivyopo Nansio,
Ukereweakiwa ameongozana na Makamu Mwenyekiti, Hawa Mwaifunga, Katibu,
GraceTendega, Naibu Katibu , Kunti Yusuph na Katibu Uenezi wa
Bavicha,Edward Simbeye.
Mdee alisema kuwa miongoni mwa wanawaharakati waliotoa tamko hilo
niwanawake aliokuwa akiwaheshimu sana toka akiwa mdogo akiamini kuwa
niwatetezi wa wanawake lakini kwa kitendo chao cha kushindwa
kusimamiamaslahi ya wanawake wenzao kimemsikitisha sana.
Alisema kuwa hoja ya uwakishi sawa 50 50 kwenye nafasi za uongozi
sikipaumbele cha wanawake wa Tanzania bali wanachotaka ni katiba
iwahakikishie upatikanaji wa huduma muhimu ikiwemo afya, elimu bora
kwa watoto wao na fursa za kiuchumi kuwa ni haki yao kikatiba
"Wanasema kuwa wanaipongeza katiba pendekezwa kwa kutoa fursa ya 50
50kwenye nafasi za uongozi hivi kweli hiki ni kipaumbele cha Wanawake
wa Ukerewe? inamsaidiaje mwanamke wa kijijini . Wanawake wanataka
katiba
iwahakikishie upatikanaji ya huduma muhimu na fursa muhimu na
wakizikosa waweze kwenda kuzidai mahakamani," alisema mwenyekiti huyo
wa BAWACHA.
AMKARIBISHA WARIOBA CHADEMA
Alisema kuwa Warioba na wazee wenzake waliokuwa kwenye tume ya Rais ya
marekebisho ya katiba wamelitumikia hili Taifa kwa uadilifu mkubwa
wala hawajaiba fedha za umma bali walichofanya ni kuamua kuweka kando
maslahi ya vyama vyao na kuhakikisha maoni ya wananchi yanazingatiwa
lakini CCM wameona hilo ni kosa na wanastahili adhabu .
" Chadema na UKAWA inawatamani kweli kweli kama chama chenu
mnachokipenda ambacho hamtaki kukihama kikiwafukuza yaani kwetu
mtapokelewa kama wafalme karibuni sana," alisema Mdee huku
akishangiliwa na wananchi.
AMSHUKIA KIKWETE NA ZAWADI YA SAA
Mdee alisema kuwa serikali imeingia mkataba wa dola za Marekanimilioni
35 sawa na zaidi ya sh. 50 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa kilometa 13
tu za reli ya umeme jiji Dar es Salaam ambapo mmiliki wa kampuni
mwenendo na usafi wake unatiliwa mashaka.
Alisema kuwa hapa nchini kuna tatizo kubwa kwa viongozi ambao wakipewa
zawadi wanasahau matatizo ya wananchi ndiyo maana wananchi
walipendekeza kwenye katiba mpya kuwa zawadi zote wanazopewa viongozi
wa umma ziwe mali ya Serikali lakini wabunge wa CCM wakayapuuza na
kuyatupa ili kuruhusu mianya ya rushwa.
"Juzi juzi tumesikia Dar es Salaam tunaletewa treni ya kwanza ya umeme
hivi nyie mnajua katika nchi hii ni asilimia 20 tu ya wananchi wa
Taifa hili ndiyo wanapata huduma ya umeme na asilimia zaidi ya 80
wakiwa kwenye giza…
"Mimi ni mkazi wa Dar suala la foleni nalifahamu na ninaelewa umuhimu
wa treni ya umeme lakini swali likaja huyu mwekezaji aliyeletwa ni
mwekezaji makini? kwasababu Watanzania mnajua jinsi mikataba ya
kifisadi ya kampuni za Richmond na Dowans zilivyoliingiza Taifa hili
kwenye giza," alisema mbunge huyo wa jimbo la Kawe.
Alisema kuwa kwa sasa kuna wizi wa fedha kwenye akaunti ya Tegeta
Escrow iliyo Benki Kuu ambapo zaiodi ya sh 200 bilioni zimechotwa
ndiyo swabau wanataka mikataba hii iwe wazi lakini CCM hawataki huku
akibainisha kuwa fedha hizo zimechotwa na CCM kwa ajili ya maandalizi
ya uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu unaotarajiwa
kufanyika mwakani.
"Tukataka tutengeneze mazingira watu wanaokuja kuwekeza kwetu wawe ni
watu wasafi si wachafu kwa sababu mchafu anatoa rushwa kwa kuwa
hajiamini sasa leo Waziri wa uchukuzi, Mwakyembe,(dk. Harrison)
kupitia kampuni ya huyu jamaa anaitwa Shumeka yaani huyu tunaambiwa ni
mwekezaji mkubwa kutoka Marekani," alisema Mdee.
Hata hivyo alisema kuwa ukienda kumtafuta kwenye Mtandaoni haumpati
yeye wala kampuni yake ya Shumoka ambapo ilipofuatiliwa zaidi
ikabaini kuwa Marekani wanasakwa kwa kuiba fedha za mifuko ya hifadhi
ya jamii
hali iliyosababisha mifuko hiyo kuwa hatarini kufilisika.
"Kumbe bwana mkubwa alivyoenda Marekani imegundulika kwamba Yule
jamaa alimpa zawadi ya saa aina ya Rolex …. ndiyo maana tukasema
viongozi wakipewa zawadi iwe mali ya Serikali ili kuepuka rushwa na
takrima kama hizi lakini magamba kule Dodoma wameifuta hili
pendekezo," alisema Mdee .
Kwa upande wake Naibu Katibu wa BAWACHA, Taifa, Kunti Yusuh,aliwataka
wanawake wa CCM kuacha kujiita wao ni Umoja Wanawake wa Tanzania,
(UWT) kwa kile alichodai kuwa si wanawake wote wa Tanzania wako kwenye
chama hicho hivyo kuanzia sasa wajiite Umoja wa Wanawake
wa CCM.
"Wameshindwa kutuletea huduma bora za afya, wameshindwa kutuhakikishia
elimu bora kwa watoto wetu, katiba haituelezi vipi tutadai haki ya
kupewa fursa zetu kiuchumi wanatuambia tutapewa nafasi 50 50 kwenye
uongozi nani kasema hiki ni kiaumbele cha wanawake wa Tanzania?,"
alihoji Kunti huku akishangiliwa na wanawake waliokuwa uwanjani hao.
MACHEMLI AFUTA MICHANGO UJENZI WA MAABARA
Kwa upande wake mbunge wa Ukerewe, Salvatory Machemli, (CHADEMA)
alisema kuwa kwenye jimbo hilo hakuna mzazi atakayechangishwa mchango
kwa ajili ya ujenzi wa maabara kwenye shule za kata kama
ilivyoagizwana Rais.
Alisema kuwa maabara hizo zitajengwa na halmashauri ya wilaya kwafedha
za kodi inayokusanywa kutoka kwa wananchi.
Alisema kuwa amemsikia Katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM, Nape Nnauye
akisema kuwa kama katiba imepita basi watashinda kwenye chaguzi za
serikali za mitaa maeneo mengi nchini jambo alilodai kuwa kama
walichakachua katiba walipokuwa wamejifungia bungeni wenyewe
wasitarajie wananchi watakubali uchakachuzi huo kwenye uchaguzi wa
serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika desemba 14, mwaka huu.
AONGOZA MAANDAMANO KUPINGA KATIBA
Awali wananchi hao walifanya maandamano ya kupinga katiba yakiongozwa
na Mdee ambapo walikuwa wakikimbia mpaka walipofika hotelini hapo
ambapo kiongozi huyo aliwaaga kwa ajili ya kuingia hotelini hapo kwa
ajili ya kuendelea na kikao cha ndani.
Wakati akimaliza kuongea na wananchi hao ghafla kundi la viongozi wa
CCM lilifika na kuingia kwenye hoteli hiyo hali iliyowafanya wananchi
hao kuanza kupiga kelele za kuzomea na kuwaita mafisadi.
MDEE AHAMA HOTELI BAADA YA VIONGOZI WA CCM KUPANGA HAPO
Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Bawacha, Mdee alilazimika kuahama
hoteli ya La Bima aliyopanga kulala baada ya viongozi wa CCM kuingia
kwenye hoteli hiyo hali iliyowafanya wananchi kuwazomea viongozi hao
wa CCM huku wakiwaita wezi mafisadi.
Hali hiyo iliamsha sintofahamu ambapo viongozi wa Chadema walijaribu
kuwatuliza wafuasi wao bila mafanikio ambapo Mdee na msafara wake
waliamua kuhama hoteli na umati huo wa watu ulimsindikiza mpaka kwenye
hoteli ya Holiday alipolala.
SIMBACHAWENE AZITAKA TAASISI ZA UMMA KUHAKIKISHA ZINATEKELEZA SHERIA YA
USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI
-
Na mwandishi wa Dar es salaam,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. George Simbachawene, ameziagiza taasisi...
1 hour ago
0 Comments:
Post a Comment