MWENYEKITI wa Taifa wa Baraza la Wanawake Chadema, (BAWACHA), Halima
Mdee, amesababisha kusimama kwa muda kwa shughuli kwenye jiji la
Mwanza wakati akiingia jijini hapo na kupokewa na msururu mrefu wa
magari na pikipiki.
Aidha mara baada ya kumaliza mkutano kwenye viwanja vya furahisha
barabara ya Airport ilishindwa kupitika kwa zaidi ya nusu saa na
kusababisha msururu mrefu wa magari kutokana na wananchi waliokuwa
kwenye mkutano huo kuamua kumsindikiza kwa maandamano mpaka kwenye
ofisi za chama hicho zilizopo eneo la Kona ya Bwiru.
Msafara huo wa Mdee ambaye pia ni mbunge wa Kawe ulipokewa oktoba 16,
mwaka huu majira ya saa 8:00 mchana eneo la Usagara lililopo kilometa
zaidi ya 20 toka
katikati ya jiji hilo ambapo pikipiki pamoja na magari hayo yalikuwa
yakishangiliwa na kupungiwa na wananchi kwenye maeneo mbalimbali
waliyopita kabla ya kuelekea kwenye uwanja wa Furahisha.
Msafara huo ulilakiwa kwa shangwe na wananchi waliokuwa wamefurika
kwenye viwanja vya Furahisha ambao Mdee na ujumbe wake
walifanyamkutano wa uzinduzi wa ziara yao ya kuzunguka mikoa yote ya
kanda yaziwa kwa ajili ya kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa
kujiandikisha kwa ajili ya chaguzi za serikali za mitaa.
Aidha mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo wananchi
waliusindikiza msafara huo huku wakiimba nyimbo za hamasa
kuikataakatiba pendekezwa mpaka kwenye ofisi za mkoa za Chadema.
AMSHUKIA CHENGE
Akiongea kwenye mkutano huo uliohudhuriwa na umati mkubwa wa
wananchiwa Mwanza, Mdee aliwataka waipigie kura ya hapana Katiba
pendekezwakwa kile alichowaeleza kuwa mbali ya maoni ya wananchi
kupuuzwa lakini inalinda maslahi ya mafisadi.
"Chenge (Andrew) alikuwa mwanasheria mkuu wa serikali,(AG) katika
kipindi hicho mikataba mingi mibovu iliingiwa na mpaka leo inawaumiza
Watanzania, mikataba ya madini, dhahabu, mikataba ya rada
yotealiisimamia yaani haijawahi kutokea mikataba mibovu kama hiyo
popote
duniani …
"Leo tunaambiwa ndiye mtu aliyependekezwa kuongoza Kamati ya
uandishiwa katiba pendekezwa, kwenye rasimu iliyowasilishwa na tume ya
JajiWarioba, (Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Joseph)
aliweka
maoni yenu wananchi mliyotaka kuwe na uwazi, uwajibikaji na
uadilifukatika uongozi ili kudhibiti mali za umma lakini kamati ya
uandishiwakaona kitawabana wakakiondoa," alisema Mdee.
Alisema kuwa mapendekezo mengine yaliyoondolewa ni zuio la viongozi wa
umma kuwa na akaunti nje ya nchi ambapo ilipendekezwa kama ni muhimu
basi iwepo sheria kali kuzidhibiti jambo alilodai kuwa ilionekana kuwa
mwiba kwa viongozi wengi wa CCM wakaamua kuitupa.
"Wananchi walichoshwa na tabia ya wale wanaoona muda wa uchaguzi
umekaribia wanakuja kutafuta kura wakishachaguliwa wanabeba mabegi yao
wanarudi mjini…
"Wananchi walitaka wapewe mamlaka ya kuwawajibisha kwa waondoa
wawakilishi ambao hawaonekani jimboni badala ya kusubiri kwa miaka
mitano lakini Chenge na wenzake wakaona itawabana wakatupilia mbali,"
alisema Mdee.
Alisema kuwa suala la Ardhi si la Muungano na katiba ya Zanzibar iko
wazi kwenye hilo kwani Mtanganyika haruhusiwi kumiliki ardhi lakini
jambo la kushangaza ni kuwa masuala ya ardhi yameingizwa katika katiba
pendekezwa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Naye Makamu Mwenyekiti wa BAWACHA Taifa, Hawa Mwaifunga, aliwataka
wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari a mkazi siku 21 kabla
ya uchaguzi wa serikali za mitaa unaotazamiwa kufanyika desemba 14
mwaka huu.
"Hao wanaopita kwa sasa na madaftari huko kuandikisha majina ni
wazushi tu, msikubali wawaandikishe kwa sababu hii kazi
inatakiwakufanywa na atendaji wa serikali na si mabalozi wa ccm
wakataeni tena siku za kujiandikisha zimeainihwa kabisa bado
hazijafika," alisema Mwaifunga.
Kwa upande wake Katibu wa BAWACHA, Grace Tendega alisema kuwa serikali
inapaswa kuelewa kuwa wananchi wameamka vya kutosha hivyo hata mbinu
za kutaka kuchakachua kura kwenye serikali za mitaa hazitafanikiwa.
Alisema kuwa uamuzi wa kusema kuwa kwenye zoezi la upigaji kura
wananchi watapaswa kuchora nembo ya chama kwenye karatasi hizo halina
nia njema hata kidogo huku akionya kuwa hila hizo haziwezi kufanikiwa.
Viongozi hao wa BAWACHA wako kwenye ziara ya mikoa ya kanda ya Ziwa
ambapo wamenga kuwahamasisha wananchi kupiga kura ya hapana dhidi ya
katiba pendekezwa na kuwahamasiha wananchi kujiandikisha kwa ajili ya
uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika Desemba 14,.
Mwakahuu.
WAZIRI CHANA AZINDUA MIRADI YA UTALII YA MILIONI 904 SERENGETI
-
Na Jane Edward, Serengeti
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amezindua
miradi ya kuendeleza utalii ikiwemo Mradi y...
2 hours ago
0 Comments:
Post a Comment