Nimefatilia kipindi cha Star TV leo asubuhi, Tuongee Asubuhi,
kilichosimamiwa na Yvonne Kamutu na Mzee Angalieni Mpendu, wakialika
Mh JJ Mnyika na Habib Mchange studio za Dar es Salaam na Mwanza kukiwa
na mgeni mmoja aliyejitambulisha ni Kada wa CHADEMA.
Nianze kwa kutabanaisha nilichokiona
Kijana Habib Mchange analazimisha bado ni mwanachama wa CHADEMA ingawa
ana Kadi ya ACT, alijibiwa unapokuwa na kadi ya chama kingine ile ya
zamani huwa ina kuwa imekufa unaweza kuwa nayo kwa kumbu kumbu lakini
kikatiba umepoteza uanachama wa chama cha awali. Mchange Habib
anasumbuliwa na msongo wa mawazo kitaalamu huitwa Emotional and
Psychological Trauma (EPT). Hali hiyo husababishwa na mihangaiko ya
kifikra za kushindwa (struggling with upsetting emotions). Moja ya
dalili ya wazi, ni kukasirika haraka, kuwa na mawazo mafupi (Myopic),
kukosa usingizi (Insomnia), kuchoka bila sababu (fatigue) n.k. Kama
ulifatilia kipindi aliomba awashiwe AC wakati Kiyoyozi kilikuwa
kinafanya kazi, Mzee Mpendu alikuwa ndani ya koti, na Mnyika
hawakulisikia lile Joto, that's abnormality! Kusema Police
walivalishwa magwanda wa polisi wamuuwe Mwangosi, that's insanity as
well, nchi hii ifanye kazi za polisi pamoja na vifaa vyao na magari
that's is myopic thinking. Mtu yeyote mwenye akili timamu angeliona
hilo. Nina amini Mchange huenda na msikitini na uwongo ni dhambi
kwenye imani ya kiislam, kuamua kuwa muongo pasi hata kuogopa Mungu
hili ni tatizo. Anadai Mnyika alikuwa Tarime uhalisia tarehe hizo
Mnyika alikuwa Zambia, kule kukasirika na kuingilia mazungumzo ni
ugonjwa wa kiakili nilioutaja Mvurugano wa maono. Sidhani kama CCM na
tawi lao ACT kama Mchange atafaa kuwa kwenye propaganda machinery zao.
Dhambi ya Usaliti inamtesa na itaendelea mtesa daima. Ndoto zake
hazijatimia, alitamani ubunge hawezi upata, alisema kwenye kipindi
Kura alizozipata Kibaha 40.000 CDM wanapata Mil 3 kama ruzuku hili
sina uhakika nalo! Anajutia nafsi yake. Anahubiri uwongo ambao hata
yeye anajua ila lazima atekeleze anachotumwa na walio nyuma ya pazia.
Mchange ana wasi wasi kwa kitu asichokijua (fear of unknown) kutokana
na mgandamizo wa chuki za kushindwa ishi ndoto zake anahijihisi hayuko
salama ndiyo maana anadai anawatafuta CHADEMA kama wanavyomtafuta
yeye. Taasisi kama CDM haiwezi hangaika na Mchange hata siku moja, CDM
kinashughulikia hoja za kitaifa ie Ufisadi na Katiba kwa sasa.
Mvurugano wa maono unamsumbua kusema Lissu, Mbowe na Mnyika wamewauwa
Shilimbe, Mwangosi, na Wangwe bila kuthibitisha ni dalili tosha kijana
anaangamia.
Anaweza kutafuta wataalamu wa Emotional and Psychological Trauma
wamsaidie vinginevyo atajikuta anakuwa adui wa nafsi yake na hata
uadui wa wale wanaomtuma. Siasa za kisasa ni kujenga hoja ujinga kila
mwenye akili anauona.
AMVUNJA MBAVU MKE WAKE KWA WIVU WA MAPENZI
-
Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi linamsaka Hamidu Abdalah kwa kosa la
kumjeruhi kwa kumpiga na chaga ya kitanda mke wake Amina Athuman Said 40,
mkazi wa Likon...
6 hours ago
0 Comments:
Post a Comment