MCHAKATO WA KATIBA - TLS WAKIMBILIA MAHAKAMANI

>
> CHAMA cha sheria Tanganyika(TLS),kimevunja ukimya na kutangaza kusudio
> la kwenda mahakamani kupinga mchakato wa katiba unaoendeshwa na upande
> mmoja katika bunge la katiba bila kuwepo kwa kundi la 201
> linalowakilishwa na umoja wa katiba ya wananchi (ukawa).
>
> Kauli hiyo imetolewa na rais wa chama hicho,Charles Rwechungura wakati
> akizungumza na vyombo vya habari jijini hapa, na kueleza kuwa tayari
> wameunda jopo la mawakili mahili watano watakaoongozwa na wakili
> kiongozi ,Kaba Mpoki kuwasilisha shauri hilo.
>
> Alisema mjibu maombi katika shauri hilo mmoja wapo atakuwa mwanasheria
> mkuu wa serikali,Fredrick Werema na wengine ambao chama hicho
> hakijawaweka wazi.
>
> ''tunaenda kuomba tafsiri ya mahakama kwa hati ya dharula lengo ni
> kuona iwapo katiba bora itapatikana''alisema .
>
> Aliongeza kuwa kusudilo hilo linalenda kuitaka mahakama itoe ufafanuzi
> wa kisheria iwapo kama upo uwezekano wa kuendelea na mchakato wa
> katiba kama kuna makundi mawili yanayosigana katika bunge la
> katiba,huku kundio moja kisusia na kutoshiriki.
>
> ''tumeamua kwenda mahakamani kutaka ufafanuzi wa kisheria kama
> tunaweza kupata katiba halali bila kuwepo kundi lingine katika
> mchakato huo''alisema Rwechungura
>
> Adha alisema tayari hati ya kusudio hilo ipo tayari baada ya tamko
> hilo kuridhiwa na wanachama wote wa chama hicho wanaokadiliwa kufikia
> 4000 .
>
> ''Sisi kama wanachama tumeona tusiweke msimamo yetu isipokuwa
> tuwasilishe mahakamani maombi ya tafsili ya vifungu, na moja wapo
> ambacho tunanuia kiwepo kwenye mawasilisho ni kifungu cha 25 cha
> sheria ya kutunga katiba ambacho kinaeleza ni madaraka gani bunge la
> katiba litakuwa nayo katika kujadili mswada wa pili''alisema
> Rwechungura
>
> Naye kaimu Afisa mtendaji mkuu wa TLS,Gura Alphonce aliwataka wananchi
> watulie kwani kamati iliyoundwa inafanya mchakato wa kuwasilisha hoja
> yao mahakamani.
>
> Hata hivyo alisema bado chama hicho hakijafikia mwaafaka kujua ni
> mahakama ipi inayohusika kufikishwa shauri hilo kati ya Zanzibar au
> Bara.
>
> ''bado kamati haijaamua itapeleka shauri hilo mahakama ipi kwa sasa,
> ni mapema sana kuwafahamisha ila kamati bado zinajadiliana na
> waandishi wa habari mtajulishwa itakapokuwa tayari''alisema
>
> Kwa upande wa wakili kiongozi tawi la Arusha,Modest Akida alisema kuwa
> kisheria hawawezi kuomba kusimamishwa kwa mchakato wa katiba bila
> kuwasilisha shauri mama la kutaka tafsili ya sheria kwanza.
>
> Katika hatua nyingine Akida alisema kuwa TLS haifungamani na upande
> wowote katika makundi mawili yanayosigana juu ya muundo upo wa
> serikali unaofaa kwa katiba mpya, hata hivyo alisema kila mwanachama
> wa chama hivyo anao uhuru wa kupendekeza ni serikali ipi anayoihitaji.
>

0 Comments:

Post a Comment