Mh Rais , bila shaka utakuwa unaifahamu
vizuri historia ya Farao - LEMA
Mh Rais nakusalimu .
Ni usiku wa manane wakati naanza kuandika
waraka huu , nimetoka kuangalia historia ya
maisha ya Dr Martin Luther Jr na nilipotaka
kulala nilishindwa na nilipotafakari jambo
jema la kufanya wakati huu nilipokosa
usingizi ndipo wajibu huu muhimu wa
kuandika waraka huu kwako ulipoanza .
Mh Rais , bila shaka utakuwa unaifahamu
historia ya Farao na Wana wa Israel wakati
Mungu alipotaka kuwatoa wana wa Israel
utumwani Misri , kwa wale Wakristo
wanaosoma Biblia wanajua kuwa , maandiko
yanasema " Na Mungu akaufanya moyo wa
Farao kuwa mgumu ili apate kujitukuza
mbele ya wana wa Israel . Mh Rais siwezi
kuandika sana juu ya nini kilitokea kwa Farao
na Watu wake ila nikuombe sana umuombe
Mch G. Rwakatare hakueleze kwa ufasaha ili
upate kujifunza jambo muhimu hapa .
Mh Rais , ukiona unafanya au unatenda hila
au dhambi bila kipingamizi wala taabu ,
maana yake ni kuwa mauti kwako
yamekaribia kwani mwizi aliyeambiwa kuwa
siku zake ni arobaini kama angeacha uovu
katika siku ya thelasini na nane pengine
angeponywa na wito wa mauti.... Nchi hii
haiko salama hata kidogo , hali ni tete sana
na kwa bahati mbaya Watawala hamuoni
kwani macho yenu yamepigwa upofu na
shetani na ndipo andiko la Godbless Lema
litatimia " Na Mungu akaufanya Moyo wa
Kikwete na ccm kuwa mgumu ili apate
kuikomboa Tanzania "
Mh Rais sina mashaka na Uhuru wa kweli na
wa pili wa Taifa ili katika siku chache
zinazokuja ,, , hamtaweza kuzuia mabadiliko
hata kama wanayoyataka sasa watakufa wote
leo , ila kukosa hekima katika uongozi
kunaweza kusabisha mabadiliko haya yakaja
na hasara kubwa katika Jamii . Hata hivyo
kiburi mlichonacho kinasababishwa na wajibu
na mipango ya Mungu katika Nchi yetu .
Mh Rais , Watu wameendelea kuteseka kila
kona , maisha ni magumu , mfumuko wa bei
umepoteza thamani ya fedha , Wagonjwa
mahosiptalini wanakufa kwani panadol
imekuwa dawa ya kutibu maradhi yote, jela
kumejaa masikini na wanyonge na Watu
wanaokwepa kodi na kulibia Taifa wamekuwa
marafiki wa watawala , ajira hakuna na vijana
wamekata tamaa , dada zetu wamekuwa
malaya wa kutafuta chakula cha siku na ada
ya kuendelea na masomo .
Mh Rais , pamoja na rasilimali tele tulizonazo
kama vile dhahabu , Tanzanite , Gesi ,
Almasi , Mbuga za Wanyama , Madini ya
Urani , Mlima Kilimanjaro , Kahawa , Pamba ,
Korosho , Bandari , Mito na maziwa na vitu
vingine vingi , bado vimeshindwa kutoa
mwanga wa maendeleo katika Taifa hili .
Mh Rais , Tuko katika kipindi ambacho
tunaandika Katiba ambayo wakati Wananchi
wanatoa maoni walikuwa na matumaini
makubwa . Mtafaruku uliopo sasa ni kati ya
UKAWA na ccm , sio vita rahisi hata kidogo
lakini Watu wajinga wanaweza kukushauri
vibaya na ukafikiri unyenyekevu kwenye
jambo hili ni kujidhalilisha , Wewe ni Rais ,
ukishindwa kutambua Mamlaka yako na
nguvu zako katika kusimamia ukweli na haki
basi Nchi itakuwa imepoteza dira . Mh Rais
unapaswa kushuka na kuwa mnyenyekevu
kwani dhamira njema yenye malengo mazuri
haiwezi kumdhalilisha binadamu . Wasira .
Lukuvi na Werema na wengine watakushauri
nakukuambia ukilihairisha Bunge utawapa
Kichwa UKAWA na Nchi itaenda Upinzani .
Mh Rais ukiitwa mpumbavu kwa ajili ya haki
na kweli , upumbavu huo una maana kubwa
kuliko kusifiwa na watu wanaopenda dhuluma
na hila hata kama ni wengi , ninahisi
changamoto unazopitia kama Rais na
Mwenyekiti wa Chama , lakini Mtu Hodari
na shujaa ni yule anayeshinda majaribu
na taabu wakati usio muaafaka .
Nakuomba ufanye maamuzi kwa ajili ya
Watoto wa watoto wa Rizwan na Watanzania
na sio Chama chako . Chama chako
kitakuwepo leo na siku moja hakitakuwepo
lakini Watoto na Wajukuu zako watakuwepo .
Hivyo basi isaidie Tanzania kupata Katiba
ambayo itampa binadamu yeyote haki ,
usawa na fursa katika Taifa lake.
Mh Rais , karibu kila mtu mwenye akili
timamu amesema juu ya jambo hili hakuna
atakaye kulazimisha lakini wakati ukifika
wakati utakulazimisha , Polisi wetu na Jeshi
halitaweza kushindana na kulishinda Jeshi
linaloitwa WAKATI , hali itakuwa ni mbaya ,
Watoto wataitafuta Tanzania na kuikosa ,
ndipo watu wazima watasema tulikuwa wapi
wakati misingi ikiharibika ? zitakuwa ni siku
za taabu na uchungu na UKAWA
hawatakuwepo tena ila WAKATI watakuwepo
na hawatamsilikiza mtu yeyote , nyumba za
kifahari na magari yanayokusanywa sasa kwa
hila na wizi hayatakuwa makazi ya Watu
isipokuwa popo na mende , Marekani ,
Uchina na Ulaya watawageuka watawaita
wahalifu wa demokrasia na wauaji ,
watawatafuta ,watawakamata na Maisha yenu
yatakuwa ya Uchungu mkubwa wakati Nchi
haitakuwepo , mimi sio mtabiri kama
marehemu Sheikh Yahaya , lakini najua
kwamba ukiwa na mwanamke mjamzito ndani
ya nyumba ni bora na ni muhimu ukaanza
kuandaa vifaa muhimu vya mtoto kama nguo
nk .
Mh Rais , sikutishi , ila Mungu hadhiakiwi
apandacho mtu ndicho avunacho , najua
watakuja wapambe hapa watakuambia
umeona ujinga wa yule Mbunge wa Arusha ?
watasema ameandika ujinga , watakebehi na
kudharau kama kawaida yao . Hata mimi
siandiki kutafuta sifa kwani mke wangu na
watoto wangu wanatosha kunisifu na kila siku
wanafanya hivyo asubuhi na jioni hasa pale
ninapowaletea Ice Cream .
Mh Rais , nisikuchoshe sana , ila tafakari
tena , natambua mara kwa mara huwa
unakuja Arusha lakini sijawahi kuambiwa wala
kutaarifiwa pengine ningekuambia haya
mambo kwa mdomo na mara nyingi huwa
nakutana na msafara wako barabarani na
ndipo natambua kuwa huko Jimboni kwangu .
Hata hivyo tunaendelea kupambana vizuri
kujenga demokrasia ya kweli na Chama chako
kinaendelea kudhoofika vizuri sana hapa
Arusha na tunatarajia kumaliza uchaguzi
Mkuu wa 2015 wa Jimbo letu hili mwaka huu
mwezi wa kumi na mbili .
Mh Rais , naomba nitoke nje ya mada yangu
muhimu kidogo , matukio ya Ugaidi na
mauaji bado yanaendelea hapa Arusha , lakini
sina taarifa za ndani sana kwani na siku
nyingi kidogo sijatembelea matajiri wa Arusha
ambao Rpc anawapa taarifa zaidi za matukio
yanayotishia usalama wa Jimbo langu kuliko
mimi Mbunge hata kama nikizihitaji kwa
barua , ni jambo la kusikitisha lakini ni jaribu
ambalo tumeweza kulisitahimili , nitajaribu
kwenda kuwaona matajiri hawa siku chache
zinazokuja ili nipate taarifa za hali ya usalama
ya Jimbo langu na nitakuandikia waraka
mwingine kukueleza ukweli , hata hivyo kuna
watu waliokamatwa hivi sasa ila kwa vile sina
taarifa za kutosha nina shindwa kujua vizuri
kama watu ha ni wahalifu au la , isipokuwa ni
na imani Mungu , Shetani na Polisi wa Arusha
wanajua vizuri .
Mh Rais , nakushukuru na ninakuombea kwa
Mwenyezi Mungu wakati unatafakari tena
kuhusu mchakato wa Katiba , hata hivyo
Watanzania wasiogope kwani " Na Mungu
akaufanya Moyo wa Kikwete na ccm kuwa
mgumu ili apate kuikomboa Tanzania "
Godbless J Lema (MB)
BASHUNGWA AIAGIZA TANROADS KUFUNGA MIZANI MITATU YA KUPIMA UZITO WA MAGARI
TUNDUMA.
-
-Ashuhudia foleni kubwa ya Malori Tunduma
-Atoa mwezi mmoja ujenzi wa kituo cha maegesho Chimbuya kukamilishwa
-Aagiza upembuzi kufanyika ili kujenga bara...
2 hours ago
0 Comments:
Post a Comment