MAMBO ndani ya Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM, (UV CCM) mkoani Arusha imezidi kuwa si shwari baada ya kikao cha baraza lao la mkoa kumkataka katibu wa CCM Mkoani hapa, Mary Chatanda kuacha kuwaingilia .Aidha, wamemtaka ahudhurie vikao vya kikatiba vinavyomtambua kama mshauri wa jumuiya hiyo na atimize majukumu yake ya ulezi bila kubagua kwa madai kuwa mivutano ndani ya jumuiya hiyo imekuwa endelevu na inataka kufanana na ile ya Palestina na Israel.Hayo yalisemwa juzi kwa nyakati tofauti na Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Robinson Meitinyiku na Katibu wa karatu , Ally Rajab wakitoa msimamo na maazimio ya kikao chao cha siku moja .Meitinyiku alisema kuwa ameshangazwa na kusikitishwa na hatua ya Chatanda alivyoamua kuzungumzia suala la mgogoro baina ya kamati ya utekelezaji ya UV CCM Mkoa na Katibu wao, Gerald Mwadalu bila kutoa fursa ya kuwasikiliza."Kama kweli mlezi wetu alikuwa na nia njema nasi ni kwa nini aliruhusu ama kutomshauri huyu Kaimu Katibu kutokwenda polisi kunishtaki mpaka pale atakapotuita? Nimewahi kujiuliza UV CCM Mkoa huu tatizo lake huwa ni nini?"Manake tumekuwa kama Israel na Palestina ni lazima ifike mahali wakubwa wa chama waone namna ya kusaidia hili, manake haiwezekani kila siku Jumuiya hii tu ndiyo inakuwa na tatizo hata mpaka wabadhirifu wanaonekana wana haki."Ninyi waandishi ni mashahidi wakati wa kuomba kura tulishughulikiwa kwelikweli, sasa hata wakati wa kutumikia vijana na kusemea ilani nako tushughulikiwe?" alihoji Meitinyiku.Akisoma maazimio 16 ya kikao hicho, Rajab alisema kuwa wamemteua, Daniel Kiyongo kukaimu nafasi ya katibu wa UV CCM mkoa kwani hawako tayari kuendelea kufanya kazi na kaimu katibu wao, Mwandalu waliyedai kuwa aheshimu viongozi, amekuwa akikwepa kuitisha vikao halali kutokana na kukabiliwa na tuhuma za ubadhirifu wa fedha na amempeleka Mwenyekiti wao polisi.Alisema kuwa wameunda kamati ndogo kufuatilia taarifa za mapato yatokanayo na vitega uchumi vilivyo chini ya jumuiya hiyo na endapo kutabainika ubadhirifu uliofanywa na Mwadalu basi watamburuza mahakamani.Pia waliwataka wafanyabiashara walio kwenye majengo yao kulipa kodi kupitia benki kwenye akaunti maalum watakayoifungua kwani awali hawakuwa na akaunti hivyo fedha hizo zilikuwa zikilipwa ofisini.Hata hivyo walishindwa kueleza ni kiasi gani cha fedha kilichopotea.Pia waliazimia makatibu wa wilaya za Ngorongoro, Raphael Ngotiek, Meru, Msafiri Mayeye, Arusha Mjini, jamal Khimji na Longido, Sakaya Kabati ambao hawakuhudhuria kikao hicho waitwe kwenye kikao cha kamati ya utekelezaji ili waeleza sababu zilizowapelekea kufikia uamuzi huo.Kwa upande wake Katibu wa CCM Mkoani hapa, Chatanda alipopigiwa simu ili atolee ufafanuzi masuala hayo alisema yupo kwenye kikao.Naye Kaimu Katibu wa UV CCM, Mwadalu alipopigiwa simu na kuelezwa juu ya yaliyoamuliwa na kikao hicho ikiwemo tujuma za ubadhirifu alijibu kwa mkato kuwa hana cha kueleza ambapo alipotakiwa afafanue kama zina ukweli alimjibu mwandishi kuwa utaamua mwenyewe
Tuzo ya Mwalimu Nyerere Yaongeza Hamasa kwa Waandishi wa Kiswahili
-
TUZO ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu itaendelea kuchochea
uandishi na usomaji hapa nchini na kuchangia kukuza lugha ya Kiswahili.
Hayo yames...
59 minutes ago