Leo Watanzania wanasubiri kuambiwa majukumu ya ACT kwa CCM ni yapi?

Habib Mchange Kwenye press conference yako leo saa 4 asubuhi jibu
uhusika wako wa kuwa wakala wa CCM ukiwawakilisha wenzake wa ACT!

Wale madiwani wa Chadema Shinyanga walitoa tuhuma nyingi. Usiishie
kujitetea suala la kulipua chopa tu!

unatakiwa kueleza vikao vilivyokuwa vikiitishwa na viongozi wa CCM
kupanga mikakati na wewe ukiwakilisha wenzako wa ACT kupewa maagizo
pale pale mbele ya madiwani namna ya kwenda kutekeleza dhidi ya
Chadema ikiwemo kwenda kuhonga, kununua na kurubuni viongozi wa
Chadema kwa nia ya kutaka kukidhoofisha bila mafanikio.

Vikao vilifanyika Hoteli ya Karena, Shinyanga, New Mwanza Hotel,
hoteli moja pale Buguruni na Kebby's Hotel ambapo alikuwepo Kitila,
Msafiri Mtemelwa na wakamtaja hadi M2 ni nani!

Hizo ni tuhuma nzito ambazo zimethibitisha bila shaka kabisa kuwa
mipango na mikakati inapangwa na viongozi wa CCM na Serikali yake
wakiwemo Kinana, Mwigulu, Makamba, Masele na Nape halafu watekelezaji
ni hao wanaojiita chama cha siasa ACT kumbe ni tawi jipya la CCM!

Habib Mchange usikwepe hilo!

0 Comments:

Post a Comment