JAMBAZI sugu anayetumia ushirikina katika kufanikisha matukio ya
uhalifu mkoani hapa,ameuawa kwa kuteketezwa kwa moto na wananchi wenye
hasira kali huku hirizi tatu alizokuwa amejifunga kiunoni zikigoma
kuungua.
Jambazi huyo ametambulika kwa jina la Devii mkazi wa Olisiva ,baada
ya kukutwa katika nyumba ya mkazi mmoja kupitia tundu dogo la dirisha.
.
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo,Emanuel Mejooli ambaye alivamiwa
nyumbani kwake na jambazi huyo ,tukio hilo limetokea saa 8.30 usiku wa
kuamkia leo akiwa amelala na familia yake baada ya kusikia kishindo na
kumkuta akiwa uchi katika chumba cha watoto wake.
Alisema baada ya kumwona jambazi huyo alimtambua kwa jina la Davii
Lebahati (30)mkazi wa Kiranyi ,Olsiva wilayani Arumeru ,ambaye
alimsihi asimuue.
''kwanza nilisikia kishindo , nilipojaribu kufunua pazia la mlango
nikamwona mtu akikatiza ,niliamua kumulika na tochi ya simu ,nilimkuta
amechuchumaa katika chumba cha watoto,huku akinjoosha mikono juu na
kunitaka nisimuue''alisema.
Baada ya tukio hilo alimhoji jambazi huyo ambaye alijitetea kuwa
aliingia ndani kwa lengo la kumfanyia 'Surprise' halia ambayo
ilimlazimu kuita watu waliojikusanya na kuanza kumshambulia na baadae
walimmwagia mafuta ya petrol na kumteketeza kwa moto.
Jambazi huyo alikiri kujihusisha na matukio ya uhalifu kishirikina
katika maeneo mbalimbali hapa mkoani hapa na alieleza kuwa aliingia
katika nyumba huyo kupitia tundu dogo la dirisha alilolionyesha,
ambapo watu wote waliokuwepo walipigwa na butwaa kwani hata ngumi ya
mtu mzima haiwezi kupenya.
Wakazi wa eneo hilo akiwemo balozi wa nyumba kumi walimtambua jambazi
huyo kwa matukio ya uhalifu na kwamba amekuwa haonekani machoni kwa
watu kwa kuwa hutumia ushirikiana anapokuwa akitekeleza matukio ya
uhalifu.
Kamanda wapolisi mkoani hapa ,Liberatus Sabas amethibitishga tukio
hilo na kusema kuwa mwili wa jambazi huyo ulichukuliwa na polisi na
kuhifadhiwa katika chumba cha maiti katika hospitali ya mkoa Mount
Meru .

0 Comments:
Post a Comment