Zitto; tunaomba umhurumie kijana huyu kabla ya mtu mwingine yeyote

Kadri mipango na mikakati ya CCM inayopangwa ili itekelezwe kupitia
tawi jipya liitwalo Alliance with CCM Tanzania (ACT), mambo yanazidi
kumharibikia mtu wao Zitto kiasi cha kuendelea kuweka rehani maisha
yake ya kisiasa tangu 'alivyofukuzwa' kwa usaliti na utovu wa nidhamu
ndani ya CHADEMA.

Baada ya kujikosha kwenye kipindi cha Mikasi cha EATV kwa maneno
matupu ya kujidai mwadilifu na kiongozi, ambayo anajua hana uwezo wa
kuyaishi, watu wa maeneo mbalimbali Mkoani Kigoma wameanza 'kutapika'
nyongo walizotunza kuhusu Zitto wakisema sasa wamedhamiria kumwanika
wazi hata kumwondolea sifa anayojipachika siku zote kuwa ni msemaji
wao!

Watu wa Kigoma wamesema kuwa wanachukizwa zaidi na watu wanaoharibu
sifa ya Mkoa huo ambao tangu kuanza kwa mfumo wa Vyama vingi umekuwa
moja ya ngome kama si nguzo ya upinzani nchini.

Kombora la kwanza (litakwenda kwa series)

Katika hatua ya kwanza wamemtaka Zitto kabla hajawadanganya Watanzania
kuwa anawahurumia dhidi ya jambo lolote ukiwemo ufisadi unaofanywa na
CCM na mawakala au washirika wao (waliopandikizwa upinzani) aanze
kuonesha huruma kwa kijana aliyemchukulia vyeti vyake na amevipoteza
matokeo yake sasa hana mbele wala nyuma.

Iko hivi; kuna Mwalimu mmoja Jimbo la Kigoma Kaskazini ambako Zitto
alikuwa akilala wakati wa kampeni za uchaguzi uliomwingiza bungeni kwa
mara ya kwanza.

Mwaka 2013 mdogo wake Mwalimu huyo alimaliza VETA, Zitto akachukua
vyeti vya kijana huyo kwa maelezo kuwa yeye ni Mkiti wa Kamati ya
Bunge ya Hesabu za Serikali na Mashirika ya Umma hivyo atamtafutia
kazi kwenye mashirika hayo bila tatizo.

Hadi leo si tu kwamba kazi haijapatikani wala hakuna dalili (maana
simu hazipokelewi au not reachable) bali pia vyeti vimepotea.

0 Comments:

Post a Comment