BOMU LAJERUHI NANE KWENYE MGAHAWA ARUSHA


www.woindeshizza.blogspot.com
  Deepak Gupta (25)
akiwa amelazwa  katika hospitali ya seliani ndani ya  chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) mara baada ya kukatwa mguu wake  wa kushoto
kutokana na mguu huo kujeruhiwa vibaya kwa bomu.


 Mtoto   Manci  Gupta akiwa amelala anasikilizia maumivu ya miguu  aliyoumia mara baada ya kulipukiwa na bomu yeye na familia yao wakati wameenda kupata chakula cha usiku katika mgahawa huo
  Munisha Gupta (42)na mme wake,Mahush
Gupta (42) akiwa wameegemeana wote wamezurika katika mlipuko wa bomu
hilo wakati wameenda kupata chakula cha usiku
 picha ikionyesha askari wa jeshi la wananchi  kitengo cha mabom wakiwa
katika eneo la tukio ambalo bumu lilirushwa  ndani ya mgahawa wa
ujulikanao kwa jina la Traditional Indian Cusine  ulipo pembeni ya
hotel ya gmkana

 muonekano wa eneo la tukio


 SEHEMU ambayo inasemekana bomu  lilitua mara baada ya kutupwa




Mkurugenzi wa tiba  wa hospitali ya Seliani Dr. Paulo akiongea na waandishi wa habari


Watu nane wamejeruhiwa kwa kitu kinachodhaniwa kuwa bomu lilolotupwa kwenye mgahawa wa Dhawa uliopo mbele ya gymkhana club jijini Arusha.

 


Alisema kuwa walipokea wagonjwa nane ambao waliumia sana katika maeneo ya miguu ambapo alibainisha kuwa katika wagonjwa hao na ne kuna mmoja ambaye aliletwa akiwa na hali mbaya sana kitu ambacho kiliwalazimu kumfanyia upasuaji usiku huo huo.





“kati yawagonjwa hao nane mmoja aliletwa akiwa mahututi sana kwani mguu wake ulikuwa umeadhiriwa sana na bomu hilo hivyo ikatulazimu  kumkata mguu mmoja wa kushoto ,mgonjwa huyo, Deepak Gupta (25) mwanaume na sasa hivi anaendelea vyema kidogo na yupokatika chumba cha ICU ndani ya hospitali hii yetu ya Seliani”alisema Kisanga





Alisema kuwa  katika majeruhi au nane aliowapokea wanawake wako watatu huku wanaume wakiwa watano na kubainisha kuwa wote wameshafanyiwa upasuaji na wapo wodini kwa ajili ya uangalizi wa madaktari





Aidha aliwataja majeruhi hao kwa majina kuwa ni pamoja na  Vinod Suvesh(37), Ritwik Khandelval (13),Raj Rajin(30),Prateck Saver,manci Gupta(14) ,Manisha Gupta (36),Mahush Gupta(42) pamoja na Deepak Gupta (25)  wote wakiwa na asili ya kiasia


Kisanga alisema kuwa kwa mujibu wa wagonjwa hao walio  waliofika hapo hospitali walidai kuwa   bomu hilo lilirushwa kwa kupitia dirishani.

0 Comments:

Post a Comment