WANANCHI jamii ya wafugaji wanaoishi karibu na Bwawa la Engaruka lenye magadi, wana hofu kuhusu mradi wa uchimbaji magadi unaotarajiwa kutekelezwa kwa ubia kati ya serikali na kampuni binafsi.
Wakazi hao wa Wilaya ya Monduli, mkoani Arusha wanadai kwamba mbali na bwawa hilo kuwapatia maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, pia mifugo yao hupata maji ya kunywa.
Hadi sasa wao na viongozi wao hawajajua ni eneo gani hasa litakalotumika kwa ajili ya kuchimba magadi hayo kama ni ndani ya ziwa au ni maeneo ya pembeni.
Wanasema viongozi wanadai wako tayari kutoa eneo la magharibi ya bwawa kwani upande wa mashariki hutumika na wanakijiji pamoja na mifugo.
Wananchi hao wanasema hayo kwa nyakati tofauti walipokuwa wakizungumza na mwandishi wa habari hizi aliyefika kwenye bwawa hilo na kushuhudia wafugaji wakifika hapo na makundi ya mifugo wakiwemo ng'ombe, mbuzi na kondoo kwa ajili ya kuwapatia maji.
http://www.freemedia.co.tz/daima/hofu-ya-mradi-wa-magadi-engaruka/
0 Comments:
Post a Comment