Mkurugenzi wa Puku, Meck Mbwana akizungumzaTANZANIA imetajwa kuwa nchi
ya pili katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, kwa manunuzi na
utumiaji wa simu za smartphone ikitanguliwa na Afrika Kusini.
Mkurugenzi wa kampuni ya bidhaa ya Puku, Meck Mbwana, alibainisha hayo
jijini Dar es Salaam juzi wakati wa hafla ya uzinduzi wa kifaa hicho
ambacho hutumika katika kuchaji simu za aina hiyo.
Alisema jambo hilo ndiyo sababu kubwa iliyowafanya kutambulisha Puku
katika nchi hii kwa bara la Afrika, ambapo awali walilenga kuuza
katika masoko ya Ulaya, hususani Marekani.
Alisema sababu nyingine ni kuweka uzalendo mbele, kwani asilimia 75 ya
umiliki wa kampuni hiyo ni Watanzania huku asilimia 25 ikiwa ni
Wamarekani.
Rais wa Puku Tanzania, Joseph Sikare, alisema pamoja na kuwepo kwa
kifaa kama hicho kinachotengenezwa na makampuni mengine, wao wamekuja
tofauti kwa kutengeneza kitu chenye ubora zaidi, mvuto kimuonekano na
kinachodumu kwa muda mrefu.
Balozi wa Puku, Happiness Magese, aliwataka Watanzania kuwaunga mkono
Puku, kwa maelezo kuwa wanatangaza utalii wa Tanzania duniani kupitia
kifaa hicho ambacho jina lake ni aina ya mnyama wa swala anayepatikana
Tanzania pekee.
TRA YATOA ELIMU MFUMO MPYA WA IDRAS
-
Farida Mangube, Morogoro
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) inatarajia kuanza rasmi matumizi ya Mfumo
Jumuishi wa Usimamizi wa Ukusanyaji wa Mapato ya Nda...
3 hours ago
0 Comments:
Post a Comment