DENI LA TAIFA LIMEVUNJA REKODI, LINATISHIA UCHUMI, USALAMA WA NCHI, DALILI YA KUFILISIKA

unaweza kupakua viambatanishwa na kujisomea docs tatu muhimu, Hotuba
ya Mpango wa Maendeleo kama ilivyosomwa na Msemaji Mkuu wa Kambi ya
Upinzani Ofisi ya Rais- Uratibu na Uhusiano, Esther Matiko, Hotuba
Bajeti Mbadala ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kama ilivyosomwa na
Waziri Kivuli wa Fedha, James Mbatia na docs nyingine inayoonesha
utoafuti kati ya Bajeti ya Kambi ya Upinzani na Bajeti ya Serikali ya
CCM.

DENI LA TAIFA
1. Mheshimiwa Spika, Deni la Taifa limeongezeka kwa kasi kubwa sana,
hali ambayo inatishia ustawi wa taifa kama halitasimamiwa kwa umakini
na haraka. Hotuba ya Waziri wa Fedha inaonesha kwamba hadi kufikia
Machi 2014, Deni la Taifa lilifikia shilingi trilioni 30.563
ikilinganishwa na shilingi trilioni 23.674 la Machi 2013. Hili ni
ongezeko la takribani trilioni 7 ambayo ni sawa na ongezeko la
asilimia 29 kwa kipindi cha mwaka mmoja tu.

2. Mheshimiwa Spika, hili ongezeko la mikopo ya takribani shilingi
trilioni 7 kwa mwaka mmoja tu, halijawahi kutokea katika historia ya
nchi yetu. Ongezeko hili la takribani trilioni 7 ni sawa na bajeti
nzima (full budget) ya mwaka 2008/9 ambayo ilikuwa ni shilingi
trilioni 6.839. Ikumbukwe kuwa mwaka 2008/9 ni miaka mitano tu
iliyopita. Ukopaji wa namna hii unatishia uchumi na usalama wa nchi.

3. Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa ripoti za Benki Kuu na hotuba
za bajeti za miaka iliyopita za Mawaziri wa Fedha, deni la Taifa
limeongezeka kwa kasi kutoka shilingi trilioni 9.3 mwaka 2007/8 hadi
shilingi trilioni 30.6 mwaka 2013/14. Hii ni wazi kuwa deni
liliongezeka kwa kiasi cha shilingi trilioni 21.3. Serikali imelipa
shilingi trilioni 4 na kufanya fedha zilizokopwa kuwa jumla ya
shilingi trilioni 25.3 katika kipindi hicho cha miaka saba tu. Huu ni
ukopaji hatarishi kwa uchumi wa taifa letu.

4. Mheshimiwa Spika, licha ya deni hili kuwa hatarishi kwa uchumi
wa Taifa, Serikali bado inatajaria kuongeza deni hilo kwa kukopa
shilingi trilioni 4.3 kama ilivyoainishwa katika bajeti ya mwaka
2014/15.

5. Mheshimiwa Spika, Serikali imeonesha kushindwa kulipa deni hilo
kwa kutumia vyanzo vyake vya mapato, badala yake imekuwa ikikopa ili
kulipa deni. Mfano hotuba ya bajeti ya mwaka 2014/15 imeonesha kuwa
katika shilingi trilioni 1.8 zilizokopwa katika soko la ndani, zaidi
ya shilingi trilioni 1.1 zilitumika kulipa madeni ya hati fungani
wakati shilingi trilioni 0.69 tu ziliwekwa kwenye miradi ya maendeleo.
Hiki ni kiashiria cha karibu sana kwa serikali kufilisika. Kukopa
mikopo ya kibiashara yenye riba kubwa ili kulipa mikopo yenye riba
ndogo au kwa uendeshaji wa kawaida wa serikali au taasisi zake ni
kiashiria cha kutosha kuainisha maamuzi yasiyo na uelewa wa kawaida
sana wa utawala na usimamizi wa fedha. (basic business and economic
sense). Mikopo ya kibiashara hutafutwa kwa matumizi ya uwekezaji wenye
lengo la uzalishaji.

6. Mheshimiwa Spika, katika uchumi unaokuwa kwa wastani wa asilimia
kati 6.5 na 7 kwa mwaka, ni vigumu sana kuweza kulipa deni la Taifa
linalokua kwa wastani wa asilimia kati ya 15 na 30 kwa mwaka. Bila
kuwa na vyanzo vipya vya mapato au kusamehewa deni hili itakuwa
vigumu sana kuweza kulipa deni hilo kikamilifu. Hii ni kwa sababu
uwiano wa ukuaji wa uchumi hauendani na kasi ya ukuaji wa deni hata
kidogo. Pamoja na upungufu wote huu, Serikali imeendelea kujitapa kuwa
inakopesheka, na hivyo kuashiria kutokuwepo na hofu yeyote ya kukopa
huku holela.

7. Mheshimiwa Spika, kinachosikitisha zaidi ni kuwa sehemu kubwa ya
mikopo hii inakopwa katika soko la ndani. Hali hii imekuwa ikileta
ushindani mkubwa kwa wananchi na wajasiriamali wanaotaka kukopa ili
kukuza mitaji. Hali hii hufanya riba za mabenki kushindwa kushuka na
hivyo kuwaathiri wakopaji na uchumi wa nchi kwa ujumla. Kwa maneno
mengine, serikali imekuwa inazuia wajasiriamali wasikope kwa riba za
bei nafuu, hivyo kufanya baadhi ya wanaokopa kwa riba zilizopo, ambazo
ni kubwa kufilisiwa. Hali hii hurudisha biashara nyuma na inainyima
serikali fursa ya kukuza uchumi na kukusanya mapato zaidi.

8. Mheshimiwa Spika, mataifa mengi duniani yanakopa na yana madeni
makubwa. Suala la msingi la kutofautisha nchi moja na nyingine ni
kasi ya kukua kwa deni husika na matumizi ya mkopo huo. Kambi Rasmi ya
Upinzani Bungeni inauliza na kutaka majibu kutoka kwa Serikali
matumizi ya fedha zilizokopwa na nchi yetu ndani ya miaka 7 ni yapi na
yameleta maendeleo kiasi gani kwa Taifa ( value for money).
naweza kupakua viambatanishwa na kujisomea docs tatu muhimu, Hotuba ya
Mpango wa Maendeleo kama ilivyosomwa na Msemaji Mkuu wa Kambi ya
Upinzani Ofisi ya Rais- Uratibu na Uhusiano, Esther Matiko, Hotuba
Bajeti Mbadala ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kama ilivyosomwa na
Waziri Kivuli wa Fedha, James Mbatia na docs nyingine inayoonesha
utoafuti kati ya Bajeti ya Kambi ya Upinzani na Bajeti ya Serikali ya
CCM.

This is an extract...

DENI LA TAIFA
1. Mheshimiwa Spika, Deni la Taifa limeongezeka kwa kasi kubwa sana,
hali ambayo inatishia ustawi wa taifa kama halitasimamiwa kwa umakini
na haraka. Hotuba ya Waziri wa Fedha inaonesha kwamba hadi kufikia
Machi 2014, Deni la Taifa lilifikia shilingi trilioni 30.563
ikilinganishwa na shilingi trilioni 23.674 la Machi 2013. Hili ni
ongezeko la takribani trilioni 7 ambayo ni sawa na ongezeko la
asilimia 29 kwa kipindi cha mwaka mmoja tu.

2. Mheshimiwa Spika, hili ongezeko la mikopo ya takribani shilingi
trilioni 7 kwa mwaka mmoja tu, halijawahi kutokea katika historia ya
nchi yetu. Ongezeko hili la takribani trilioni 7 ni sawa na bajeti
nzima (full budget) ya mwaka 2008/9 ambayo ilikuwa ni shilingi
trilioni 6.839. Ikumbukwe kuwa mwaka 2008/9 ni miaka mitano tu
iliyopita. Ukopaji wa namna hii unatishia uchumi na usalama wa nchi.

3. Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa ripoti za Benki Kuu na hotuba
za bajeti za miaka iliyopita za Mawaziri wa Fedha, deni la Taifa
limeongezeka kwa kasi kutoka shilingi trilioni 9.3 mwaka 2007/8 hadi
shilingi trilioni 30.6 mwaka 2013/14. Hii ni wazi kuwa deni
liliongezeka kwa kiasi cha shilingi trilioni 21.3. Serikali imelipa
shilingi trilioni 4 na kufanya fedha zilizokopwa kuwa jumla ya
shilingi trilioni 25.3 katika kipindi hicho cha miaka saba tu. Huu ni
ukopaji hatarishi kwa uchumi wa taifa letu.

4. Mheshimiwa Spika, licha ya deni hili kuwa hatarishi kwa uchumi
wa Taifa, Serikali bado inatajaria kuongeza deni hilo kwa kukopa
shilingi trilioni 4.3 kama ilivyoainishwa katika bajeti ya mwaka
2014/15.

5. Mheshimiwa Spika, Serikali imeonesha kushindwa kulipa deni hilo
kwa kutumia vyanzo vyake vya mapato, badala yake imekuwa ikikopa ili
kulipa deni. Mfano hotuba ya bajeti ya mwaka 2014/15 imeonesha kuwa
katika shilingi trilioni 1.8 zilizokopwa katika soko la ndani, zaidi
ya shilingi trilioni 1.1 zilitumika kulipa madeni ya hati fungani
wakati shilingi trilioni 0.69 tu ziliwekwa kwenye miradi ya maendeleo.
Hiki ni kiashiria cha karibu sana kwa serikali kufilisika. Kukopa
mikopo ya kibiashara yenye riba kubwa ili kulipa mikopo yenye riba
ndogo au kwa uendeshaji wa kawaida wa serikali au taasisi zake ni
kiashiria cha kutosha kuainisha maamuzi yasiyo na uelewa wa kawaida
sana wa utawala na usimamizi wa fedha. (basic business and economic
sense). Mikopo ya kibiashara hutafutwa kwa matumizi ya uwekezaji wenye
lengo la uzalishaji.

6. Mheshimiwa Spika, katika uchumi unaokuwa kwa wastani wa asilimia
kati 6.5 na 7 kwa mwaka, ni vigumu sana kuweza kulipa deni la Taifa
linalokua kwa wastani wa asilimia kati ya 15 na 30 kwa mwaka. Bila
kuwa na vyanzo vipya vya mapato au kusamehewa deni hili itakuwa
vigumu sana kuweza kulipa deni hilo kikamilifu. Hii ni kwa sababu
uwiano wa ukuaji wa uchumi hauendani na kasi ya ukuaji wa deni hata
kidogo. Pamoja na upungufu wote huu, Serikali imeendelea kujitapa kuwa
inakopesheka, na hivyo kuashiria kutokuwepo na hofu yeyote ya kukopa
huku holela.

7. Mheshimiwa Spika, kinachosikitisha zaidi ni kuwa sehemu kubwa ya
mikopo hii inakopwa katika soko la ndani. Hali hii imekuwa ikileta
ushindani mkubwa kwa wananchi na wajasiriamali wanaotaka kukopa ili
kukuza mitaji. Hali hii hufanya riba za mabenki kushindwa kushuka na
hivyo kuwaathiri wakopaji na uchumi wa nchi kwa ujumla. Kwa maneno
mengine, serikali imekuwa inazuia wajasiriamali wasikope kwa riba za
bei nafuu, hivyo kufanya baadhi ya wanaokopa kwa riba zilizopo, ambazo
ni kubwa kufilisiwa. Hali hii hurudisha biashara nyuma na inainyima
serikali fursa ya kukuza uchumi na kukusanya mapato zaidi.

8. Mheshimiwa Spika, mataifa mengi duniani yanakopa na yana madeni
makubwa. Suala la msingi la kutofautisha nchi moja na nyingine ni
kasi ya kukua kwa deni husika na matumizi ya mkopo huo. Kambi Rasmi ya
Upinzani Bungeni inauliza na kutaka majibu kutoka kwa Serikali
matumizi ya fedha zilizokopwa na nchi yetu ndani ya miaka 7 ni yapi na
yameleta maendeleo kiasi gani kwa Taifa ( value for money).

0 Comments:

Post a Comment