WATAFITI WAENDA KWA BABU KUTAFITI AINA YA DHAHABU INAYOCHIMBWA

 

MKUU wa Wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali, amesema kuwa wataalam wa madini wanaendelea na utafiti kubaini endapo madini yanayoendelea kuchimbwa na wananchi kwenye maeneo ya milima na mtoni kwenye kijiji cha Samunge ni dhahabu.

 

Aidha amekanusha taarifa zilizozagaa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuwa kuna ongezeko kubwa la watu kwenye kijiji hicho toka maeneo mbalimbali ya nchi tokea kubainika kuwepo kwa dhahabu hiyo katikati ya mwezi machi mwaka huu kwa madai kuwa wageni hawazidi asilimia 5.

 

Aliyasema hayo jana alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jijini Arusha ambapo alisema kuwa wataalamu hao kutoka aofisi ya madini kanda ya kaskazini wanatazamiwa kumpatia matokeo ya utafiti huo wakati wowote kuanzia jana mchana.

 

WawaLali alisema kuwa hakuna madini yanayookotwa juu ardhi bali yanachimbwa bali yanachimbwa huku akionya kuwa huenda upotoshaji huo uinfanywa ili kunufaisha badhi ya watu ikiwemo kijiji hicho ambacho hutoza sh 10,000 kwa kila amtu anayeingia.

 

 

 

Hata hivyo alisema kuwa baada ya matokeo ya wataalam wa madini kutolewa na ikibainika ni madini ya aina gani yanayopatikana Samunge basi Serikali itatoa muongozo juu ya namna ya kuyachimba ili kuepuka maafa yanayoweza kujitokeza endapo watu wataachwa kuchimba holela kama ilivyo sasa.

 


Alifafanua kuwa hakuna watu 4,000 kwenye kijiji cha Samunge kama inavyoelezwa na baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya jamii kwani kwa mujibu wa tathmini iliyofanyika kijijini hapo inaonyesha kuna watu wanaochimba madini hayo ni kati ya 500 hadi 600 na kati yao wenyeji wa kijiji hicho ni asilimia 80.

 

Mkuu huyo wa wilaya ya Ngorongoro alisema kuwa wengine asilimia 10  wanatoka ndani ya kata ya Samunge na tano wanatoka Wilayani Ngorongoro na asilimia tano tu ndiyo wanaotoka nje ya kata ya Samunge.

Alisema Serikali imeimaruisha ulinzi kwenye eneo hilo kwa kuongeza mgambo wa kutosha na Polisi sanjari na kuboresha mazingira a ya eneo husika kuhakikisha huduma muhimu za vyoo vinapatikana ili kuepuka mlipuko wa magonjwa ya mlipuko  kama wakati wa kikombe cha babu.

Alionya kuwa  eneo hilo linakabiliwa na tatizo la uhaba mkubwa wa maji kwani wanachanzo kimoja tu cha maji jambo alilodai kuwa  endapo hakutakuwa na usimamizi kwenye shughuli za
uchimba madini na kuyaosha kunaweza kutokea mgogoro

 

 

 



 

 

0 Comments:

Post a Comment