MAHAKAMA Kuu Kanda ya Arusha imeiamuru Halmashauri ya wilaya ya Arusha kuwalipa fidia wananchi 43 wanaoishi kandokando ya barabara ya mianzini mpaka Timolo ili wapishe upanuzi wa barabara hiyo yenye umbali wa kilomita 8.
Aidha imeagiza atafutwe mthamini binafsi ili afanyie tathmini ya mali zilizoendelezwa ili zoezi la ulipaji fidia lifanyike kwa kuzingatia thamani halisi ya mali zilizoendelezwa na wananchi hao 43 wa Vijiji vya Kiding`a, Moivo, Kirevi, Sambasha na Kiranyi wilaya ya Arumeru.
Uamuzi huo umetolewa mwanzoni mwa wiki na jaji, Fatma Masengi, aliyekuwa akisikiliza shauri la ardhi namba 18 / 2013 lililofunguliwa wananchi hao kupitia wakili wao, Modest Akida.
Alisema kuwa amefikia uamuzi huo baada ya kupitia hoja za msingi na ushahidi wa pande zote na kuridhika bila shaka kuwa barabara hiyo iliwakuta wananchi hao hivyo wanahaki kulipwa fidia ili kupisha upanuzi wake.
Uamuzi huo ulipokewa kwa furaha na wananchi hao ambapo mwenyekiti wao, Fanuel Lamai, alisema kuwa wanaona haki imetendeka kwani mwanzo walikuwa na mashaka kutokana na vitisho na ubabe walivyokuwa wakifanyiwa na viongozi wa halmashauri hasa madiwani.
"Ilifika wakati baadhi ya wenzetu tuliofungua nao kesi hii waliamua kurudi na kuvunja nyumba zao wenyewe kutokana na vitisho vilivyokuwa vikiendelea, lakini sasa tuna amani kabisa na tuna uhakika wa kulipwa haki zetu," alisema Mwenyekiti huo.
Wakili wa wananchi hao,Akida alisema kuwa ameridhika na uamuzi huo kwani haki imetendeka.
Kwa upande wake wa mwanasheria wa halmashauri, Jonathan Kiama, alisema kuwa hana pingamizi na uamuzi huo wa mahakama ingawa kwa sasa hawana mpango wa kupanua barabara hiyo kwa upana wa mita 15 ambayo sheria yake ya mwaka 2007 ndiyo iliyowakuta wananchi hao.
Alisema kuwa kwa sasa mpango wao ni kupanua kwa upana wa mita 10 jambo alilodai kuwa upana huo hautafika kwenye nyumba na mali za wananchi hao.
Kwenye shauri hilo upande wa waleta maombi walileta mashahidi watano huku upande wa wajibu maombi ambao ni halmashauri ukileta mashahidi mashahidi 9 ambapo mahakama ilileta shahidi mmoja ambaye ni mtaalam kutoka bodi ya wakala wa barabara nchini, (TANROADS).
Wananchi hao kupitia wakili wao, Akida walipeleka maombi mahakamani hapo ikiitaka itamke kuwa wao ni wamiliki halali wa ardhi na mali zao zilizopo maeneo ya pembezoni mwa barabara ya Mianzini mpaka Timbolo.
Pia waliiiomba mahakama hiyo iwaelekeze halmashauri ya wilaya ya Arusha iwalipe fidia ya ardhi waliyoiendeleza na mali zao yenye thamani ya zaidi ya sh biloni 3.2 ili waweze kupisha ujenzi wa barabara hiyo ya mianzini mpaka Timbolo.
DC ILALA AMALIZA MGOMO WA WAFANYAKAZI ZAIDI YA 1,500 WA KIWANDA CHA NAMERA,
GONGOLAMBOTO
-
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Edward Mpogolo, amefanikiwa kumaliza mgomo wa
wafanyakazi zaidi ya 1,500 wa Kiwanda cha NAMERA kilichopo Gongolamboto,
jijini...
2 hours ago
0 Comments:
Post a Comment