Mkuu wa wilaya ya Arusha, John Mongela akiongea kwenye Ibada ya mchana ambapo aliwataka Watanzania kuchangia mambo ya msingi ikiwemo injili na elimu tofauti na sasa ambapo hujitokeza kichangia harusi
Mkuu wa wilaya, Mongela alichangia sh. 500,000 kwa ajili kumchangia mwimbaji wa nyimbo za injili Samwel Nungwana kununua vyombo vya vya muziki.
DC Mongela akikumbatiwa na mch, Andrew Kajembe Mara baada ya kuzungumza kwenye Ibada hiyo.
Mch. Kajembe akisisitiza umuhimu wa waumini kuendelea kuombea amani ya nchi. Pia aligikisha ujumbe outplay kwa askofu wa Anglikana Daiyosisi ya mt Kilimanjaro , Stanley Hotaye akimuomba DC kukumbusha utekelezJi wa mapendekezo 10 waliyopeleka kwa Rais Jakaya Kikwete kwa ajili ya utekelezaji kwa ajili ya mustakabali mwema wa Amani ya jiji la Arusha
KANISA la Anglikana, St James, Kaloleni, wamefanya ibada maalum ya kuombea mchakato wa katiba mpya pamoja na ulinzi wa Mungu kwa waandishi wa habari na viongozi wa serikali mkoani Arusha.
Maombi hayo yalifanyika juzi kwenye ibada zote nne zilizofanyika kanisani hapo na kuhudhuriwa na waandishi wa habari mbalimbali ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha, John Mongela.Ibada hizo ziliongozwa na Mchungaji kiongozi wa kanisa hilo, Andrew Kajembe ambaye pia aliombea uwepo kwa amani, uzalendo, haki na mapatano hapa nchini.
Alimuomba Mkuu wa Wilaya, Mongela, kuhakikisha mapendekezo 10 yaliyotolewa na wadau wa amani ya mkoa wa Arusha kwa lengo la kuhakikisha kunakuwa na amani ya kudumu yanamfikia, Rais Jakaya Kikwete ili yaweze kuingia kwenye utekelezaji ingawa hakuyataja.
“Kwa niaba ya Askofu wangu, Stanley Hotay, ambaye ni Mwenyekiti wa Maaskofu wa Arusha, napenda nikupe salamu za kumfikishia RPC, (kamanda wa polisi mkoa), kuwa sisi (taasisi za kidini) tayari tumeshateua wajumbe 10 kwa ajili ya kuingia kwenye kamati ya ulinzi na usalama kama tulivyokubaliana, hivyo tunasubiria wito wake tu ili tumpelekee majina hayo,” alisema.
Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya, Mongela aliwataka wananchi kubadilika kwa kuachana na mazoea mabaya ya kuweka kipaumbele katika kuchangia harusi na badala yake waanze kuchangia mambo ya msingi ikiwemo elimu na masuala ya maombi.
“Tutoke kwenye kuchangia vitu ambavyo baada ya muda mchache vinapotea, mnielewe sisemi msishiriki kwenye masuala ya jamii zenu, ila mshirikiane na kwenye masuala ya msingi kama kupata ada na shughuli za maombi kama hizi,” alisema Mongela.
Sent from my iPhone
0 Comments:
Post a Comment