TIRA KANDA YA KASKAZINI YAANDAA TAMASHA KUBWA LA ELIMU YA BIMA CHUO CHA UHASIBU ARUSHA .

 



Happy Lazaro Arusha.

MAMLAKA ya usimamizi wa Bima (TIRA) kanda ya kaskazini imeandaa Tamasha kubwa la elimu ya bima na michezo katika chuo cha uhasibu Arusha kwa lengo la kujengea uwezo kuhusu maswala ya bima ambapo zaidi ya wanafunzi mia tatu wamehudhuria tamasha hilo .




Akizungumza kwenye hafla hiyo jijini Arusha leo Meneja wa Bima kanda ya kaskazini Dokta Emmanuel Lupilya amesema kuwa, kupitia tamasha hilo wanafunzi hao wameweza kupata elimu kuhusu maswala mbalimbali ya Bima na kuweza kuzijua faida za kukata bima mbalimbali.



Dkt.Lupilya amewaasa wanafunzi waliopo vyuo mbalimbali nchini kuhakikisha swala la bima haliepukiki kwani ndio uti wa mgongo katika kuhakikisha uchumi unajengwa sio tu kwa fedha bali kwa misingi ya kuwekeza kwenye bima kukinga mali afya pamoja na jamii yote kwa ujumla wake.



"jamii inayofundishwa na kuelimishwa juu ya elimu ya bima hakika serikali yake haiwezi kubeba mzigo mzito wa majanga hivyo tunahamisha hayo majanga kuelekea kwenye makampuni ambayo tunayasajili sisi kama mamlaka ili kuona kuwa shughuli zote za uchumi kijamii zinazoendeshwa na wananchi zinaenda kukingwa na bima ."amesema Dkt.Lupilya.



Amesema kuwa ,mamlaka ya Bima ipo kwa ajili ya kukinga ndoto za wadau wote wakiwemo jamii,wanafunzi ,na ndicho kimewafanya kufika chuoni hapo kutoa elimu upande wa bima na michezo ili michezo iwaandae vijana hawa kuwa wabunifu na weledi katika maswala ya kuonesha ukomavu kwenye uongozi kwa baadaye .



"Tumeanza leo kwenye chuo cha uhasibu Arusha lakini ndoto zetu ni kufika mikoa na wilaya zote ambazo tunazisimamia kupitia Kanda hii ya Kaskazin ."amesema .




Aidha ametaja matarajio yao ya baadaye ni kufikia walengwa zaidi hususani jamii ambayo haijafikwa na bima na kuweza kufika vijijini na hata maeneo ambayo wanananchi wanahitaji huduma hiyo ya bima .


"Tumepanga utaratibu wa kuwafungulia wakala ambao utakuwa ni shirikishi kwa maana ya chuo wanakuwa na uwakala ili shughuli zote za kusimamia maswala ya kijamii katika chuo hiki.ziweze kufanikiwa, tutahakikisha makampuni yetu yanatengeza bidhaa ambazo zinajibu changamoto ambayo imekuwa kubwa katika nchi yetu na kuondokana na utegemezi kuomba fedha kila wakati na kuona namna ambavyo bima itasaidia nchi na kusonga mbele na kuhakikisha ndoto za hawa wanafunzi zinafikiwa ."amesema Dkt.Lupilya.



Kwa upande wake Afisa bima kutoka Tira Goodluck Massawe amesem kuwa ,lengo la kuandaa tamasha hilo kwa wanafunzi hao ni ili waweze kuwa mabalozi wazuri wa kueneza ujumbe huo wa maswala ya bima popote wanapokwenda .



Massawe amesema kuwa,wanafunzi zaidi ya Mia tatu wamejitokeza kupata elimu ya maswala ya bima ambapo kupitia tamasha hilo ambalo limeleta hamasa kubwa sana wameweza kuwafikia watu wengi zaidi.


"Natoa wito zaidi kupitia Tamasha hili wanachuo na wananch kwa ujumla wajue umuhimu wa kukinga mali zao dhid ya majanga kupitia Bima na kulinda afya zao kwakuwa na bima ."amesema .


Amesema lengo la kufika chuoni hapa ni utaratibu wao kama Mamlaka kwa ajili ya kutoa elimu hivyo kundi hili la chuo ni moja ya wadau ambao wanafanya nao kazi kwa karibu sana na lengo kubwa ni kuwandaa kuwa mabalozi wazuri katika kuwafikia wananchi kupitia utoaji Elimu ya bima ili kuendeleza SOKO la bima nchini.


Nao baadhi ya wanafunzi walioshiriki tamasha hilo ,Abdalah Juma na Jenifa Jeremiah wamesema kuwa kitendo kilichofanywa na Tira ni mfano wa kuigwa na makampuni mengine kwani wameweza kuwajengea uelewa mkubwa kuhusu maswala ya bima na kuahidi kubwa mabalozi wazuri wa kwenda kutangaza elimu hiyo popote watakapokuwa.



0 Comments:

Post a Comment