MGEJA: Urais haujaribiwi, Dk. Samia anatosha



Na Mwandishi Wetu 

Kahama na Nzega


KADA maarufu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na mwanasiasa mkongwe, Khamisi Mgeja, amewatahadhalisha watanzania wasifanye makosa kumchagua rais asiye na uzoefu kwani nafasi hiyo haijaribiwi.



Amesema yatakuwa makosa makubwa kuchagua wagombea wasio na uzoefu wa

kiuongozi ambao hawajawahl kufanyakazi yeyote hata za serikali za mitaa wakati mgombea urais makini wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan yupo na anatosha



Mgeja alisema hayo leo tarehe 27 Oktoba wakati wa mikutano ya kampeni kwenye maeneo tofauti ya wilaya ya Nzega, mkoani  Tabora na wilaya ya Kahama mkoni Shinyanga wakati akiwanadi wagombea

ubunge jimbo la Nzega, Hussein Bashe na Benjamin Ngayiwa wa jimbo la Kahama Mjini



Mgeja aliwakumbusha watanzania wosia 

wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliyewahi kusema " Kiongozi bora wa nchi yetu hawezi kutoka nje ya CCM bali atatoka ndani ya CCM" na mgombea huyo ni Dk. Samia Suluhu Hassan ambaye ndiye chaguo sahihi la Watanzania.


Akiwa wilayani Kahama katika kijiji cha Nyanhembe na Ufala, Mgeja amewaomba

 wananchi  wachague Bashe na Ngayiwa kuwa wabunge, Betha Daud kuwa Diwani na

 Dk. Samia kuwa rais wa nchi.


" Tuna kila sababu ya kumuunga mkono mama yetu Dk. Samia Suluhu Hassani kwani kafanya mambo mengi sana ya kimaendeleo katika nchi yetu, kila sekta za kimaendeleo amezigusa katika mafanikio makubwa sana na mifano ipo hai na inajieleza. Sisi tuna wajibu wa kumlipa kura za heshima na kishindo hiyo tarehe 29 kwenye boksi la kura. Tujitokeze kwa wingi, twende tukatiki," alisema Mgeja.


Kuhusu wagombea ubunge, Mgeja alisema mgombea  Benjamini Ngayiwa  bado ni kijana mwenye ari  kubwa ya kuwatumikia wananchi wa jimbo la  Kahama Mjini, hivyo aliwaomba wananchi wamuunge  mkono kwa kumchagua ili afanyekazi ya kuleta maendeleo katika jimbo hilo.


Akiwa  katika  jimbo la Nzega, Mgeja alimmiminia sifa Mbunge wa jimbo hilo, Bashe kwamba watanzania wameridhika na utendaji wake kama Waziri wa Kilimo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.


Aliwapongeza wana CCM na wanaanchi wa jimbo la Nzega kuendele kumuunga mkono Bashe kwani ni chaguo sahihi kwao na kwa maslahi mapana ya jimbo la  Nzega. 


Alisema Bashe ni mmoja wa wabunge vijana wachapa kazi na mwenye maono makubwa kwani amefanya 

mambo makubwa katika jimbo la Nzega na bado ana mengi ya kuyafanya kwa wananchi wa jimbo hilo.


Mgeja alimwelezea  Dk. Samia kuwa ni Mama aliyejaa imani ya utu katika nafsi yake, hivyo apewe kura za  kishindo kwani amefanya kazi iliyotukuka na ana amini yajayo yanafurahisha zaidi.


Kuhusu umoja na ushikamano wa taifa,  Mgeja amewambia wananchi kuwa upo imara na nchi iko salama chini ya Rais Samia.


Amewaomba wananchi waendelee kuwa na imani na CCM na wasikubali kurubuniwa na wanaochochea chuki wakiwa nchi za nje wakitumiwa na mabeberu kutaka kuleta vurugu nchini


0 Comments:

Post a Comment