Wagombea 16 Wathibitishwa kuwania Ubunge Jimbo la Arusha Mjini

 


Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Arusha Mjini, Shabani Manyama, ametangaza kuwa jumla ya wagombea 16 wamethibitishwa kuwania nafasi ya ubunge kupitia vyama mbalimbali vya siasa, baada ya zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu kukamilika rasmi Jumatano, Agosti 27, 2025 saa kumi jioni.

Zoezi hilo lilianza Agosti 14, 2025 saa 1:30 asubuhi na kufungwa kwa mujibu wa ratiba ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).

Kwa mujibu wa Manyama, vyama vilivyowasilisha wagombea wao ni pamoja na CCM, ACT-Wazalendo, CHADEMA, CUF, NLD, DP, UDP, NRA, TLP, UPDP, UMD, CCK, AAFP, Sauti ya Umma, Makini na CHAUMMA. Aidha, alibainisha kuwa Chama cha ADC kilishindwa kurejesha fomu na hivyo hakitashiriki katika kinyang’anyiro hicho.

Wagombea waliothibitishwa ni:

  1. Paul Christian Makonda – CCM

  2. Amina Mkombozi Mhina – ADA Tadea

  3. Simon Johnson Bayo – Sauti ya Umma

  4. Msifuni Goffrey Mwanga – TLP

  5. Alfred Nicolas Mollel – NLD

  6. Simon Paul Ngilisho – Chama cha Demokrasia Makini

  7. Zuberi Mwinyi Hamisi – CUF

  8. Musa Amosi Ayo – DP

  9. Mark Manasse Diganyeka – UMD

  10. Mgina Ibrahimu Mustafa – AAFP

  11. Daniel Shehiza Daffa – UDP

  12. Rashid Jaralya Mkama – NRA

  13. Magdalena Said Masaka – UPDP

  14. Ramadhan Sephu Bigo – CCK

  15. Said Salim Njuki – ACT-Wazalendo

  16. John Benjamin Lema – CHAUMMA

Ratiba ya Uchaguzi

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza kuwa kampeni za uchaguzi zitafanyika kuanzia Agosti 28, 2025 hadi Oktoba 28, 2025, na wananchi watapiga kura siku ya Jumanne, Oktoba 29, 2025.

INEC imewataka wagombea wote kuendesha kampeni kwa amani, kufuata sheria na kanuni za uchaguzi, huku ikiwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kutumia haki yao ya kidemokrasia.


0 Comments:

Post a Comment