CAG Kichere Akagua Ujenzi wa Miundombinu Kijiji cha Msomera



Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Charles Kichere, ametembelea kijiji cha Msomera kilichopo wilayani Handeni kwa lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali inayosimamiwa na Serikali.



Katika ziara hiyo, Kichere alikagua nyumba 1,500 ambazo tayari zimekamilika kwa ajili ya wananchi wanaohamia kutoka Ngorongoro kwa hiari. Pia alikagua maendeleo ya miradi ya barabara, huduma za maji, shule, vituo vya afya, umeme, pamoja na maeneo ya mifugo kama minada na malisho.



"Ni muhimu kuhakikisha fedha za umma zinatumika ipasavyo na miradi inakamilika kwa ubora unaotakiwa," alisema Kichere wakati wa ukaguzi huo.



Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Salum Nyamwese, alisema: "Serikali imefanya kazi kubwa ya kuwekeza katika kijiji cha Msomera, na sasa kimekuwa mfano wa kuigwa nchini."



Kichere aliambatana na Kamishna wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Abdul-Razaq Badru, pamoja na watendaji kutoka ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali, Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.

0 Comments:

Post a Comment