Mwalimu Amar Ajitokeza Kuwania Uongozi Kupitia CCM Tanga

 



Na Mwandishi wetu, Tanga

Joto la uchaguzi limezidi kupanda katika jiji la Tanga baada ya Mwalimu Kassim Amar kujitokeza kuchukuwa fomu kwa ajili ya kuomba ridhaa ya kuweza kuchaguliwa na wanachama wa chama cha Mapinduzi .


Amar ameweza kupewa fomu na katibu wa CCM wilaya ya Tanga Jamal Khimji mapema leo asubuhi katika ofisi za chama hicho jijj la Tanga 



Akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kuchukuwa fomu Amar amesema kuwa uongozi wa Rais Samia umemvutia kuweza kuona ipo haja kugombea ili kuunga mkono juhudi hizo .


"Nia yangu ni kuomba ridhaa kwa wanaccm kuweza kuwatumika wanatanga hivyo nawaomba waniunge mkono katika dhamira hii ya kuwaletea maendeleo wananchi wenzangu "amesema Amar.

0 Comments:

Post a Comment