PANGA PANGUA YA SAMIA YAMLETA KIHONGOSI ARUSHA DR PIMA ARESHWA TRC YAPATA MKURUGENZI MPYA

  



Dar es Salaam, 23 Juni 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko ya uongozi kwa kuwahamisha na kuwateua viongozi mbalimbali wa Serikali, ikiwemo Wakuu wa Mikoa, Makatibu Wakuu, Wakurugenzi wa Halmashauri na viongozi wengine wa ngazi za Wilaya. Taarifa hii imetolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka.

MABADILIKO YA WAKUU WA MIKOA

  • Kenan Laban Kihongosi amehamishwa kutoka Mkoa wa Simiyu kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

  • Anamringi Macha amehamishwa kutoka Shinyanga kwenda Simiyu.

UTEUZI MPYA WA WAKUU WA MIKOA

  • Simon Nyakoro Sirro – Mkuu wa Mkoa wa Kigoma

  • Kheri Denice James – Mkuu wa Mkoa wa Tanga

  • Mhoni Mohamed Mhita – Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga

  • Beno Moris Malisa – Mkuu wa Mkoa wa Mbeya

  • Jabiri Omnari Makame – Mkuu wa Mkoa wa Songwe

UTEUZI WA KATIBU MKUU

  • Onesmo Meena – Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi

UHAMISHO WA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA

  • Rachid Sichalwe – kutoka Pwani kwenda Tanga

  • Hassan Mnyera – kutoka Tanga kwenda Pwani

UTEUZI WA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA

  • Abdul Rajab Mhinte – Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam

  • Frank Hawasi – Katibu Tawala Mkoa wa Songwe

UHAMISHO WA NAIBU KATIBU MKUU

  • Hussein Mohamed Omari – kutoka Wizara ya Afya kwenda Elimu, Sayansi na Teknolojia

UTEUZI WA NAIBU MAKATIBU WAKUU

  • Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira (jina halijatajwa)

  • Mhandisi Athumani Juma Kilundanya – Kilimo (maendeleo ya mazao na usalama wa chakula)

UHAMISHO WA WAKUU WA WILAYA

  • Solomon Jonas Itunda – kutoka Songwe kwenda Mbeya

  • Ibrahimu Kubecha – kutoka Handeni kwenda Gairo

  • Amin Mohamed Mkalipa – kutoka Arumeru kwenda Ilemela

UTEUZI WA WAKUU WA WILAYA

  • Estomin Stavros Kyando – Kilolo

  • Ayubu Yasin Setabile – Muleba

  • Thecla Mkuchika – Butiama

  • Angela Marco Lubela – Serengeti

  • Maulid Hassan Dotto – Mvomero

  • Rukia Ally Zuberi – Mwanga

  • Mwinyi Ahmed Mwinyi – Arumeru

  • Jubilete Win Lauwo – Magu

  • Mikaya Tumaini Daimu – Kigamboni

  • Thomas Mendrald Mtyinga – Sikonge

  • Cloriana Tulius Kimath – Monduli

  • Upendo Bert Wella – Tabora

  • Donis Gervas Masanja – Tunduru

  • Fadhil Emanuel Nkurlu – Songwe

  • Benjamin Samuel Sitta – Iringa

  • Salum Nyamwese – Handeni

  • Frank John Mkinda – Kahama

UTEUZI WA MAKATIBU TAWALA WA WILAYA

  • Mwanamwema Kombo – Mkinga

  • Kassim Salum Kirondomara – Biharamulo

  • Thobias Abwaro – Babati

  • Asyeritus Mumens Egaruk – Meatu

  • Nyakafu Etanga Mashauri – Kilolo

  • Mustapha Ayubu Kimomwe – Rufiji

  • Milama Masiko – Serengeti

  • Mpampalika Mfaume Mpampalika – Mwanga

  • Richard Jackson Mwalingo – Mtwara

  • Zuberi Said Zuberi – Magu

  • Angela Henry Mono – Tanga

  • Mamndolwa Miraj Gembe – Same

  • Sabina Starlin Mwajeka – Momba

  • Sosthenes Chakupanyuka – Kaliua

  • Adestino Gwelino Mwilinge – Mbogwe

UHAMISHO WA WAKURUGENZI WATENDAJI WA HALMASHAURI

  • Justice Laurent Kijazi – kutoka Iringa kwenda Jiji la Mbeya

  • Zaina Maume Mlawa – kutoka Bahi kwenda Manispaa ya Iringa

UTEUZI WA WAKURUGENZI WATENDAJI WA HALMASHAURI

  • Raymond Mweli – Wilaya ya Mbarali

  • Adelina Enock Mfikwa – Wilaya ya Bukombe

  • Iddi Ally Ndabona – Mji wa Bariadi

  • Hamisi Hamidu Idd – Wilaya ya Busega

  • Mwarami Seif – Wilaya ya Nzega

  • Newaho Mkisi – Wilaya ya Meatu

  • Zainab Salum Mgomi – Mji wa Nanyamba

  • Dkt. John Marco Pima – amerejeshwa serikalini na ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Tabora baada ya kushinda kesi ya uhujumu uchumi akiwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha.

  • Albina William Mtumbuka – Wilaya ya Bahi

  • Paulo Francis Faty – Wilaya ya Mvomero

  • Shabani Kabelwa – Wilaya ya Kaliua

  • Vicent Augustino Mbua – Wilaya ya Ukerewe

UTEUZI WA MKUU WA TAASISI

  • Mhandisi Machibya Masanja – Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC)

Taarifa ya Ikulu imeeleza kuwa uapisho wa Wakuu wa Mikoa, Katibu Mkuu, Makatibu Tawala wa Mikoa na Naibu Makatibu Wakuu walioteuliwa utafanyika kwa tarehe itakayopangwa baadaye.


Imeandaliwa na:
Sharifa B. Nyanga
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

0 Comments:

Post a Comment