Wahifadhi TFS Wakagua Ukarabati wa Miundombinu ya Barabara Shamba la Mgololo

 


Wahifadhi kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kupitia Shamba la Miti Sao Hill wamefanya ukaguzi wa miundombinu ya barabara katika Tarafa ya Nne ya Shamba la Mgololo, ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha barabara ndani ya msitu huo zinaendelea kupitika kwa urahisi.



Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, mmoja wa wahifadhi alisema, "Lengo ni kuhakikisha kuwa shughuli za usafirishaji wa malighafi kutoka msituni zinaendelea kufanyika bila vikwazo, kwa kuwa barabara hizi ni muhimu kwa wavunaji wa miti."

Ukaguzi huo ni sehemu ya juhudi za TFS kuhakikisha kuwa miundombinu ya barabara inaboreshwa na inadumu, ili kurahisisha shughuli za kila siku za wadau wanaotegemea msitu huo kwa ajili ya uvunaji na usafirishaji wa miti.

Tunaendelea kushughulikia changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika Shamba la Sao Hill ili kuhakikisha kuwa wadau wetu wanatekeleza majukumu yao kwa ufanisi na bila kuchelewa, alieleza mhifadhi mwingine.

Kwa sasa, TFS kupitia Shamba la Sao Hill inaendelea na maandalizi ya bustani za miche ya miti kwa ajili ya msimu ujao wa upandaji, huku mvua zikiendelea kunyesha katika baadhi ya maeneo, hali inayowezesha shughuli hizo kufanyika kwa ufanisi zaidi.

0 Comments:

Post a Comment