Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, alisisitiza kuwa amani inapaswa kurejeshwa bila masharti yoyote, akiongeza kuwa juhudi za kumaliza vita zinahitaji ushirikiano wa pande zote. Kauli hii ilitolewa baada ya mkutano wa wakuu wa majeshi kutoka nchi zinazoiunga mkono Ukraine, ambao walikubaliana kupeleka ujumbe wa amani nchini Ukraine ili kulinda makubaliano yoyote ya kusitisha vita yatakayofikiwa.
Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer, alieleza kuwa suala la kusitisha vita sasa liko mikononi mwa Urusi, na Rais Vladimir Putin hana budi kuketi katika meza ya mazungumzo. Starmer alisema, "Mipango yoyote ya kuweka silaha chini kati ya Ukraine na Urusi ni lazima ihusishe juhudi za Marekani." Aliongeza kuwa, wakuu wa majeshi kutoka nchi zinazoiunga mkono Ukraine watakutana Uingereza kujadili mipango ya kutuma ujumbe wa amani ili kulinda makubaliano yoyote ya kusitisha vita.
Kwa upande mwingine, Kansela wa Ujerumani, Olaf Scholz, aliunga mkono wito wa kurejesha amani na kusema Urusi inapaswa kufanya juhudi za kumaliza vita vya miaka mitatu.

0 Comments:
Post a Comment