Rais Samia Kuzindua Sera ya Ardhi ya Mwaka 1995, Toleo la 2023

 

Sera hii inalenga kuimarisha usimamizi wa ardhi kwa kuongeza ufanisi wa utawala, kutatua migogoro ya ardhi, na kuweka mifumo inayosomana ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa na ufuatiliaji wa shughuli za ardhi. 


Pia, itaongeza uwazi na ushirikishwaji wa wananchi katika masuala ya ardhi, kuwezesha uwekezaji endelevu, na kulinda haki za wamiliki wa ardhi vijijini na mijini.

Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua Sera ya Ardhi ya Mwaka 1995, toleo la 2023, inayolenga kukidhi mahitaji ya sasa na kugusa masuala mbalimbali ikiwamo migogoro ya ardhi. 

Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika Machi 17, 2025, katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.



Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 15, 2025, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Deogratius Ndejembi, amesema maandalizi ya uzinduzi huo yamekamilika kwa asilimia 90 na kwamba kazi zilizobaki zitakamilika ndani ya muda mfupi.

"Kutokana na umuhimu wa suala la ardhi, miongoni mwa wageni watakaohudhuria ni pamoja na Mabalozi wa nchi mbalimbali, Wakuu wa Mikoa pamoja na Mawaziri," alisema Ndejembi.

Sera hii inalenga kuimarisha usimamizi wa ardhi, kuboresha utawala, na kudhibiti migogoro ya ardhi. Pia, itawezesha mifumo inayorahisisha upatikanaji wa taarifa na ufuatiliaji wa shughuli za ardhi. Sera hiyo pia itaimarisha uwazi, ushirikishwaji wa wananchi, na kulinda haki za wamiliki wa ardhi vijijini na mijini. Kaulimbiu ya uzinduzi huu ni "Sera ya Ardhi Msingi wa Ustawi na Malengo Endelevu ya Taifa."

0 Comments:

Post a Comment