Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi, amesema kuwa nchi yake iko tayari kuingia mkataba wa madini na Marekani, ambapo mabadilishano yatahusisha kupata uwezo wa kujilinda dhidi ya makundi ya ¹ mashariki mwa taifa hilo. Akizungumza na kituo cha televisheni cha Fox News, Tshisekedi alieleza kuwa makubaliano haya yataiwezesha Kongo kuchimba madini yake kupitia kampuni za Marekani huku ikinufaika kwa kuimarisha mifumo yake ya ulinzi na usalama.
"Tunataka kuhakikisha kuwa nchi yetu inapata uwezo wa kulinda rasilimali zake, na mkataba huu utaisaidia Kongo kufaidika kwa kujenga mifumo ya usalama na kutengeneza nafasi ya biashara ya madini na Marekani," alisema Tshisekedi.
Kongo ni taifa lenye utajiri mkubwa wa madini, ikiwemo kobalti na urani, na imekuwa ikikumbana na changamoto kubwa ya kukabiliana na kundi la waasi wa M23, linaloungwa mkono na Rwanda. Kundi hili limefanikiwa kuchukua udhibiti wa maeneo makubwa upande wa mashariki mwa nchi hiyo tangu mwanzoni mwa mwaka huu. Hivi karibuni, waasi wa M23 walishambulia na kuingia mji mdogo wa Walikale, licha ya mwito wa kusitishwa mapigano uliotolewa na Rais Tshisekedi na Rais wa Rwanda, Paul Kagame, walipokutana nchini Qatar.
Waasi wa M23 Watekua Mji wa Walikale
Taarifa kutoka Walikale zinasema waasi wa M23 waluteka mji huo Jumatano jioni baada ya milio ya risasi ya hapa na pale. Mmoja ya viongozi wa jadi wa mji wa Walikale amesema waasi hao walipenyeza ngome ya jeshi na kutumia njia mbadala kuufikia mji huo.
"Waasi wa M23 wamefanikiwa kuingia Walikale, mji ambao ni muhimu kiuchumi na kimkakati. Hii ni pigo kubwa kwa usalama wa maeneo ya mashariki mwa Kongo," aliongeza kiongozi huyo wa jadi.
Mji wa Walikale ni watatu kwa uzalishaji wa madini ya bati ulimwenguni na umeunganishwa na majimbo manne ya mashariki mwa Kongo, ambayo ni Kivu Kaskazini, Kivu Kusini, Tshopo, na Maniema. Walikale ni muhimu kwa uchumi wa Kongo na umekuwa kivutio kwa makundi ya waasi.
Tshisekedi Akosoa Waasi wa M23
Rais Tshisekedi pia alikosoa vikali hatua ya waasi wa M23 kutohudhuria mazungumzo ya amani ya Luanda yaliyofanyika nchini Angola. Alisema kwamba kutojihusisha kwa waasi wa M23 ni ishara ya wazi kuwa kundi hilo linatumiwa na Rwanda kwa maslahi yake.
"Waasi wa M23 hawakuhudhuria mazungumzo ya Luanda, na hiyo ni ishara tosha kuwa kundi hili ni vibaraka wa Rwanda. Wanafuata maagizo ya kiongozi wa Rwanda na hawana nia ya kumaliza mgogoro huu," alisema Tshisekedi.
Macron Aunga Mkono Juhudi za Amani
Juhudi za kurejesha amani mashariki mwa Kongo pia zimeungwa mkono na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, ambaye alikutana na wawakilishi wa makanisa ya Kongo mjini Paris. Askofu Fulgence Muteba, mwenye kiti wa Kongamano la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Kongo, alisema kuwa mpango wa amani wa viongozi wa kidini unalenga kuwaweka pamoja si tu serikali na waasi wa M23 bali wanasiasa wote na mashirika ya kiraia ili kufikia suluhisho la kudumu la mzozo wa Kongo.
"Ni lazima Wakongo waweke pamoja kwenye meza ya mazungumzo. Umwagaji damu hauna manufaa yoyote. Lazima tuweke tofauti zetu kando na kujenga mshikamano wa kitaifa," alisisitiza Askofu Muteba.
Tshisekedi Atayari kwa Mazungumzo na Kagame
Tshisekedi alieleza kuwa yuko tayari kwa mazungumzo zaidi ya moja kwa moja na Rais wa Rwanda, Paul Kagame, baada ya mkutano wao wa hivi karibuni mjini Doha, Qatar. Alisema kuwa upatanishi uliofanywa na Qatar umeonyesha dalili za matumaini, lakini aliendelea kukosoa hatua ya waasi wa M23 na kusema kuwa ni muhimu waasi hao waonyeshe nia ya kweli ya kumaliza mapigano.
"Upatanishi wa Qatar umeonyesha busara, lakini hatua ya waasi wa M23 kutohudhuria mazungumzo ya amani ni uthibitisho wa wazi kwamba wao ni vibaraka wa Rwanda," aliongeza Tshisekedi.
Kufuatia hali hii, juhudi za kisiasa, kidiplomasia, na kijeshi zinahitajika ili kurejesha utulivu mashariki mwa Kongo na kuzuia mzozo huu usiendelee kutishia usalama wa kikanda.

0 Comments:
Post a Comment