Tundu Lissu Aingia Rasmi Ofisini, Atoa Wito wa Umoja na Mabadiliko ndani ya CHADEMA Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, leo ameingia rasmi ofisini kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe Januari 21, 2025.
Katika hotuba yake, Lissu amesisitiza umoja wa wanachama wa CHADEMA na umuhimu wa mabadiliko ndani ya chama na nchini kwa ujumla.
"Tumevutana sana. Tumesemana sana. Mara nyingi tumesemana sio vizuri sana. Hatujasifiana. Tumezungumza mambo yaliyo mabaya yetu," alisema Lissu huku akitilia mkazo kuwa uchaguzi umepita na sasa ni wakati wa kurekebisha palipo bomoka na kujenga upya chama. Lissu alisisitiza kuwa ushindi wa CHADEMA katika uchaguzi wa ndani ni ushindi wa wote na si wa mtu mmoja. "Wote tunasifiwa, kwani anasifiwa aliyeshinda tu? Kwani anasifiwa aliyeshindwa peke yake? Tunasifiwa wote. Tumeshinda wote." Aidha, aliwahimiza wanachama kuondokana na maneno ya chuki na mgawanyiko, akiwatahadharisha dhidi ya kauli za "tutaona watafanyaje kazi" au "kaeni mbali tumewashinda," akisema hizo ni kauli zinazoweza kudumaza mshikamano ndani ya chama. Katika hotuba yake, Lissu alikumbusha maneno ya Abraham Lincoln aliyoyasema Machi 4, 1861, aliposisitiza kuwa taifa moja haliwezi kugawanyika kwa sababu ya tofauti za kisiasa. "Hayo maneno ya Abraham Lincoln ya Machi 4, 1861 yanatuhusu na sisi, nafikiri. Hii mihemko hii, imetuvuruga vuruga sana. Lakini tusiiruhusu ivunje urafiki wetu." Kwa mujibu wa Lissu, CHADEMA inahitaji kuwa na jeshi kubwa zaidi la wanachama na wafuasi ili kufanikisha mapambano ya mabadiliko nchini. "Tunahitaji kila mtu alete talanta yake. Kila mtu alete karama zake. Kila mtu alete baraka alizojaaliwa na mwenyezi Mungu kwenye hii kazi inayo takiwa kufanyika pamoja." Lissu alieleza kwa uwazi msimamo wa CHADEMA kuhusu uchaguzi mkuu ujao, akisema, "No Reform. No Election," akifafanua kuwa chama hakitasusia uchaguzi, bali kinahitaji kwanza kufanyika kwa mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi kabla ya kushiriki. "Sio tutasusia uchaguzi. Hatujazungumza boycott. Hatujazungumza non participation. Tunasema: Hakuna Mabadiliko. Hakuna Uchaguzi." Akiendelea na msisitizo wake juu ya umuhimu wa mabadiliko, Lissu alisema: "Tutaenda kuzungumza na kila mtu mchana kweupe. Hakuna agenda ya siri. Tutaenda kuongea na marafiki zetu duniani. Tutawaambia msimamo wetu hadharani. Tutawaambia watuunge mkono." Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche, alisema chama hicho kimefanya uchaguzi wa kidemokrasia uliotoa funzo duniani na kuirejesha nchi katika zama za matumaini kama ilivyokuwa mwaka 2010. "Tumemaliza uchaguzi. Hakuna mtu atapata upendeleo kwa sababu alimuunga mkono Heche au Lissu. Tutachagua kulingana na merit," alisema Heche, akisisitiza kuwa hakuna nafasi ya visasi ndani ya CHADEMA. Heche alieleza kuwa baada ya uchaguzi wa ndani, chama kinarejea kwa wananchi kushughulikia masuala muhimu ya taifa, akisema, "Tukitoka kwenye retreat tunaingia ground. Tutaacha kushughulika na CCM kama tukiwa tumekufa." Katika kauli yake, Heche pia alimtaja mwanasiasa mkongwe wa CCM, Stephen Wassira, akisema, "Nimemuona mzee Wassira, amekuwa serikalini kwa zaidi ya miaka 60, mimi sikuwa nimezaliwa. Mzee Wassira, Lissu sio saizi yako. Lissu atashughulika na Rais. Lissu hawezi kushughulika na wewe, hakuna hiyo nafasi." Aliongeza kuwa vijana wa kizazi cha sasa, maarufu kama Gen-Z, wanakabiliwa na changamoto za ajira na siasa za zamani haziwezi kuwahadaa. "Sasa Wassira anakuja kuongea na vijana wa Gen-Z ambao hawana ajira!" Heche alisisitiza kuwa CHADEMA itarudi kwa wananchi kuwakumbusha haki zao na kuhakikisha kuwa CCM inaondolewa madarakani kwa njia halali na za kidemokrasia. "CHADEMA itawakumbusha wajibu wenu na kuwaondoa madarakani." Pia aliwataka polisi kutotishia upinzani, akisema, "Kwenu polis, msitake kututisha. Jana tulitaka tuje hapa ili mtukamate. Habari ingekuwa Heche na Lissu wakamatwa. Tukaamua kuwasamehe." Akihitimisha hotuba yake, Heche alimshukuru Mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA kwa kusimamia uchaguzi kwa uwazi na kuonyesha mfano bora wa uongozi. "Ninamshukuru sana M’kiti wetu mstaafu. Tunakupenda. We love you. M’kiti amesimamia uchaguzi transparently. Hakung’ang’ania madaraka, wengine huwa wanang’ang’ania madaraka." Kwa ujumla, hotuba za viongozi wa CHADEMA zimeonesha dhamira ya kuimarisha mshikamano ndani ya chama huku wakijipanga kwa mapambano ya kisiasa dhidi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, leo ameingia rasmi ofisini kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe Januari 21, 2025. Katika hotuba yake, Lissu amesisitiza umoja wa wanachama wa CHADEMA na umuhimu wa mabadiliko ndani ya chama na nchini kwa ujumla.
"Tumevutana sana. Tumesemana sana. Mara nyingi tumesemana sio vizuri sana. Hatujasifiana. Tumezungumza mambo yaliyo mabaya yetu," alisema Lissu huku akitilia mkazo kuwa uchaguzi umepita na sasa ni wakati wa kurekebisha palipo bomoka na kujenga upya chama.
Lissu alisisitiza kuwa ushindi wa CHADEMA katika uchaguzi wa ndani ni ushindi wa wote na si wa mtu mmoja. "Wote tunasifiwa, kwani anasifiwa aliyeshinda tu? Kwani anasifiwa aliyeshindwa peke yake? Tunasifiwa wote. Tumeshinda wote."
Aidha, aliwahimiza wanachama kuondokana na maneno ya chuki na mgawanyiko, akiwatahadharisha dhidi ya kauli za "tutaona watafanyaje kazi" au "kaeni mbali tumewashinda," akisema hizo ni kauli zinazoweza kudumaza mshikamano ndani ya chama.
Katika hotuba yake, Lissu alikumbusha maneno ya Abraham Lincoln aliyoyasema Machi 4, 1861, aliposisitiza kuwa taifa moja haliwezi kugawanyika kwa sababu ya tofauti za kisiasa. "Hayo maneno ya Abraham Lincoln ya Machi 4, 1861 yanatuhusu na sisi, nafikiri. Hii mihemko hii, imetuvuruga vuruga sana. Lakini tusiiruhusu ivunje urafiki wetu."
Kwa mujibu wa Lissu, CHADEMA inahitaji kuwa na jeshi kubwa zaidi la wanachama na wafuasi ili kufanikisha mapambano ya mabadiliko nchini. "Tunahitaji kila mtu alete talanta yake. Kila mtu alete karama zake. Kila mtu alete baraka alizojaaliwa na mwenyezi Mungu kwenye hii kazi inayo takiwa kufanyika pamoja."
Lissu alieleza kwa uwazi msimamo wa CHADEMA kuhusu uchaguzi mkuu ujao, akisema, "No Reform. No Election," akifafanua kuwa chama hakitasusia uchaguzi, bali kinahitaji kwanza kufanyika kwa mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi kabla ya kushiriki.
"Sio tutasusia uchaguzi. Hatujazungumza boycott. Hatujazungumza non participation. Tunasema: Hakuna Mabadiliko. Hakuna Uchaguzi."
Akiendelea na msisitizo wake juu ya umuhimu wa mabadiliko, Lissu alisema: "Tutaenda kuzungumza na kila mtu mchana kweupe. Hakuna agenda ya siri. Tutaenda kuongea na marafiki zetu duniani. Tutawaambia msimamo wetu hadharani. Tutawaambia watuunge mkono."
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche, alisema chama hicho kimefanya uchaguzi wa kidemokrasia uliotoa funzo duniani na kuirejesha nchi katika zama za matumaini kama ilivyokuwa mwaka 2010.
"Tumemaliza uchaguzi. Hakuna mtu atapata upendeleo kwa sababu alimuunga mkono Heche au Lissu. Tutachagua kulingana na merit," alisema Heche, akisisitiza kuwa hakuna nafasi ya visasi ndani ya CHADEMA.
Heche alieleza kuwa baada ya uchaguzi wa ndani, chama kinarejea kwa wananchi kushughulikia masuala muhimu ya taifa, akisema, "Tukitoka kwenye retreat tunaingia ground. Tutaacha kushughulika na CCM kama tukiwa tumekufa."
Katika kauli yake, Heche pia alimtaja mwanasiasa mkongwe wa CCM, Stephen Wassira, akisema, "Nimemuona mzee Wassira, amekuwa serikalini kwa zaidi ya miaka 60, mimi sikuwa nimezaliwa. Mzee Wassira, Lissu sio saizi yako. Lissu atashughulika na Rais. Lissu hawezi kushughulika na wewe, hakuna hiyo nafasi."
Aliongeza kuwa vijana wa kizazi cha sasa, maarufu kama Gen-Z, wanakabiliwa na changamoto za ajira na siasa za zamani haziwezi kuwahadaa. "Sasa Wassira anakuja kuongea na vijana wa Gen-Z ambao hawana ajira!"
Heche alisisitiza kuwa CHADEMA itarudi kwa wananchi kuwakumbusha haki zao na kuhakikisha kuwa CCM inaondolewa madarakani kwa njia halali na za kidemokrasia. "CHADEMA itawakumbusha wajibu wenu na kuwaondoa madarakani."
Pia aliwataka polisi kutotishia upinzani, akisema, "Kwenu polis, msitake kututisha. Jana tulitaka tuje hapa ili mtukamate. Habari ingekuwa Heche na Lissu wakamatwa. Tukaamua kuwasamehe."
Akihitimisha hotuba yake, Heche alimshukuru Mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA, Freeman Mbowe kwa kusimamia uchaguzi kwa uwazi na kuonyesha mfano bora wa uongozi. "Ninamshukuru sana M’kiti wetu mstaafu. Tunakupenda. We love you.
Mwenyekiti amesimamia uchaguzi transparently. Hakung’ang’ania madaraka, wengine huwa wanang’ang’ania madaraka."
0 Comments:
Post a Comment