Rais Samia: Dkt. Mpango Aomba Kupumzika, Nchimbi Mgombea Mwenza

 


Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amethibitisha kuwa Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango, amemwandikia barua ya kuomba kupumzika kwenye wadhifa wake. Dkt. Samia alisema kuwa baada ya kufikiria kwa makini ombi hilo, ameridhia lakini Dkt. Mpango ataendelea kuwa Makamu wa Rais hadi Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Akizungumza , Januari 19, 2025, katika Mkutano Mkuu Maalum uliofanyika Jijini Dodoma, Rais Samia alisema, "Dkt. Philip Mpango ndiye Makamu wa Rais. Miezi ya karibuni hapa amekuja kuniona kuniomba apumzike, ana sababu kadhaa lakini sio za kazi, anasema yeye sasa ana miaka 68 na angependa kuishi zaidi kwahiyo naomba nipumzisheni, nikambishia bishia. Wiki iliyopita hapa akanikabidhi barua yangu hii (ya kujiuzulu?) na barua sikumjibu, nilipoenda kwenye Kamati Kuu."

Kwa mujibu wa Rais Samia, Dkt. Mpango atabaki na wadhifa wa Makamu wa Rais hadi Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, ambapo atakuwa akifanya kazi kama kawaida.

0 Comments:

Post a Comment