Papa Francis Apumua kwa Oksijeni Asumbuliwa na Maambukizi ya Mapafu

 


Papa Francis, mwenye umri wa miaka 88, bado anaendelea kupokea matibabu ya dharura kufuatia matatizo ya kupumua na maambukizi tata ya mapafu. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Vatican, Papa anapokea oksijeni ya ziada na kuongezewa damu, huku uchunguzi wa kliniki ukiendelea kufanywa.

"Taarifa fupi ya mapema Jumapili haikutaja endapo Papa Francis alitoka kitandani au kupata kifungua kinywa, kama alivyofanya siku zilizopita," ilisema taarifa kutoka Vatican. Hata hivyo, taarifa iliongeza kuwa "usiku ulipita vyema na Papa alipumzika."

Taarifa zaidi kutoka Vatican zilisema kuwa "Papa Francis alikuwa na fahamu, akiendelea kupokea oksijeni ya ziada," na kwamba "uchunguzi zaidi wa kliniki ulikuwa ukifanywa." Taarifa za kina za matibabu zilitarajiwa kutolewa baadaye Jumapili.

Kwa upande mwingine, madaktari walisema siku ya Jumamosi kwamba Papa, ambaye alifanyiwa upasuaji wa pafu akiwa kijana, alikuwa katika hali mbaya baada ya kukumbwa na tatizo la muda mrefu la ugonjwa wa pumu na hivi karibuni alipatwa na pneumonia na maambukizi tata ya mapafu.

Hali ya Papa Francis inasubiriwa kwa hamu huku maombi yakiendelea kutumwa kutoka sehemu mbalimbali za dunia kwa ajili ya uponyaji wake.

0 Comments:

Post a Comment