Operesheni Kuinyanyua Meli ya MV Serengeti: Inaendelea

 



Operesheni ya kuinyanyua meli ya MV Serengeti inaendelea kufanywa kwa umakini mkubwa, baada ya meli hiyo kuzama kwenye Ziwa Victoria, Mkoa wa Mwanza, Disemba 26, 2024. 


Viongozi wa vyombo mbalimbali vya usalama, ikiwemo Jeshi la Zimamoto, wamesema kuwa hatua za dharura zinaendelea kuchukuliwa ili kuhakikisha usalama wa meli na kuondoa hatari yoyote inayoweza kutokea kwa umma na mali za serikali.




Kaimu Mkurugenzi wa TASHICO, amesema kuwa uchunguzi wa sababu za kuzama kwa meli hiyo unaendelea na hatua kali zitachukuliwa dhidi ya watu watakaobainika kuhusika na tukio hilo. Alieleza kuwa tatizo lililochangia kuzama kwa meli hiyo ni matundu ya Stain tube ambayo yalikuwa na upana usio wa kawaida, jambo lililohatarisha usalama wa meli. 


Aliongeza kwamba uchunguzi zaidi unafanyika ili kubaini wapi tatizo lilipo na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wahusika.



“MV Clarias ilikuwa na tatizo la matundu (Stain tube) yaliyo na upana usio wa kawaida, ya kuruhusu maji kuingia ndani ya meli na kupumua kwa kiwango kinachotakiwa.


 Uchunguzi unaendelea na hatua zitachukuliwa kwa wale watakaobainika kuhusika,” alisema Kaimu Mkurugenzi wa TASHICO.



Kwa upande mwingine, Said Sekiboto kutoka Kitengo cha Uokoaji Ndani ya Maji cha Jeshi la Zimamoto ya Uokoaji Mkoa wa Mwanza, ameeleza kuwa operesheni ya kuinyanyua meli imekuwa ikikumbwa na changamoto za vifaa. 


Sekiboto alifafanua kuwa vifaa walivyokuwa navyo awali havikuwa na uwezo wa kuinyanyua meli kwa haraka, lakini sasa wameimarisha vifaa hivyo na kuendelea na operesheni hiyo kwa kutumia vifaa vya ziada.



“Vifaa tulivyokuwa navyo havikuwa na uwezo wa kuinyanyua meli kwa haraka, lakini sasa tumeimarisha vifaa hivyo na tunaendelea na operesheni ya kuinyanyua. Tutatumia vifaa vya ziada kuendelea na kazi ya kuinyanyua meli na kufyonza maji yaliyokuwa yamejaa ndani pamoja na kwenye Chelezo,” alisema Sekiboto.



Sekiboto aliongeza kuwa, ingawa meli hiyo imezama upande wa nyuma, sehemu ya mbele inashikilia juu ya maji na kwamba kazi ya kuondoa maji ndani ya meli itaendelea kwa siku nzima ili kuhakikisha meli inarejea katika hali yake ya kawaida. Alisisitiza kuwa kazi hiyo ni muhimu kwa usalama wa meli na kuhakikisha kuwa hatari yoyote inayoletwa na tukio hili inaondolewa.


“Meli imezama upande wa nyuma, lakini hakuna madhara makubwa. 


Sehemu ya mbele inaendelea kuelea juu ya maji, kazi ya kuondoa maji ndani ya meli itafanyika kwa siku nzima ili kuhakikisha usalama wa meli na kuirejesha hali yake,” alisema Sekiboto.


Kwa sasa, TASHICO pamoja na vyombo vingine vya usalama wanaendelea na operesheni hiyo kwa umakini mkubwa ili kuhakikisha kuwa meli ya MV Serengeti inarejeshwa kwa usalama. 


Uchunguzi wa kitaalamu unaendelea, na hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wahusika wa tukio hili, ili kuhakikisha kuwa hatari kama hii haijirudii tena.

0 Comments:

Post a Comment