Na Gift Mongi,Dodoma
Katika kuhakikisha kuwa wanafunzi wengi wa vyuo vikuu nchini wananufaika na fedha zitolewazo na serikali kupitia bodi ya mikopo ya elimu ya juu, (HESLB) bodi hiyo imetakiwa kuongeza nguvu katika ufwatiliaji wa mikopo ambayo wamekwishaitoa ili kuweza kurejeshwa.
![]() |
Akichangia bajeti ya Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro Prof Patrick Ndakidemi alimpongeza Prof Adolf Mkenda ambaye ndiye waziri wa wizara hiyo na kuwa mwenendo kwa sasa unaridhisha.
Kwa kujibu wa Prof Ndakidemi yapo mageuzi makubwa ya kimkakati yaliyofanyika kwa kusimamia vyema elimu kuanzia shule ya msingi, sekondari na Vyuo vya kati na vyuo vikuu.
"Katika kutoa mikopo nipendekeze bodi hiyo ya mikopo ifikirie upya na kujipanga katika utoaji wa mikopo kwa kutoa kipaumbele kwa watu wa sayansi kama madaktari ili wasije kurudi nyuma kwani wataweza kulisaidia taifa kwa siku zijazo'aliaema
Prof Ndakidemi alisema kuwa kwa sasa ni dhahiri pasipo na mashaka kubwa wizara hiyo imepata mtu mchapakazi mnyenyekevu na mwenye maono ya elimu na taifa kwa ujumla wake.
Aliongeza kuwa, lengo la mzazi yeyote anayempelekea mtoto wake chuoni ni kuhakikisha kuwa anapata elimu bora, ujuzi, uzoefu na mwishoni anakuwa na mafanikio kwa kuajiriwa au kuwa mjasiriamali hivyo ni vyema taasisi zote ambazo zimepewa dhamana ya kuwapa vijana elimu zikawa zimekamilika kikamilifu.
"Mheshimiwa mwenyekiti takwimu tulizonazo kama wabunge zinaonyesha kwamba taasisi nyingi hasa za Serikali na binafsi hapa nchini hazijakamilika ambapo zinaupungufu wa hali ya juu"alisema
Alisema kuwa, kutokana na kutokukamilika kwa taasisi hizo kunaupungufu mkubwa wa Waadhiri kumepelekea ufundishaji, utafiti na kutoa huduma kwa jamii kumeathirika kwa kiwango kikubwa.
Aliongeza kuwa katika vyuo 100 bora Afrika, chuo kikuu cha Nairobi ni cha saba kwa ubora Afrika na ni cha 855 Duniani lakini Makerere ni cha 13 Afrika na ni cha 1613 Dunia, huku chuo Kikuu cha Dar es salaam(UDSM) ni cha 37 Afrika lakini ni cha 2475 Duniani huku chuo kikuu cha SUA ni cha 86 Afrika, huku Chuo cha Afya Muhimbili ni cha 95 Afrika lakini ni cha 4642 Duniani.
Alisema kuwa, katika vyuo kumi bora Afrika vyuo saba vinatoka Afrika kusini na kimoja kimetoka Afrika mashariki, huku katika vyuo 100 bora Afrika vyuo kumi vimetoka Afrika mashariki.
0 Comments:
Post a Comment