Diane Rwigara Awasilisha Fomu ya Kugombea Urais Rwanda
Leo, Diane Rwigara, mwanasiasa wa upinzani nchini Rwanda, amewasilisha rasmi karatasi zake za kutaka kugombea Urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Julai mwaka huu. Hii inakuja baada ya siku ya mwisho iliyotolewa na tume ya uchaguzi nchini humo kwa wagombea kuwasilisha maombi yao.
Diane Rwigara alipofika katika tume ya uchaguzi mbele ya umati mkubwa wa waandishi wa habari, aliwasilisha karatasi yake ya kugombea kiti cha urais kwa mwenyekiti wa tume hiyo, Bi. Oda Gasinzigwa. Alielezea matumaini yake kwamba safari hii maombi yake yatakubaliwa.
Hata hivyo, mwaka 2017, maombi yake yalikataliwa kwa madai kwamba hakukidhi vigezo vya tume ya uchaguzi, ikiwa ni pamoja na kutuhumiwa kwa kughushi saini za wafuasi. Vigezo hivyo ni pamoja na kuwa na saini za wafuasi 600 kutoka wilaya zote 30 za Rwanda.
Diane Rwigara ameonesha matumaini kuwa safari hii maombi yake yatakubaliwa, akidai kwamba safari hii amefuata taratibu zote na kutimiza mahitaji yote.

0 Comments:
Post a Comment