Kiongozi wa Upinzani, Aibuka Kuwa Rais Mpya wa Senegal
Katika uchaguzi mkuu uliofanyika hivi karibuni nchini Senegal, kiongozi wa upinzani Bassirou Diomaye Faye, mwenye umri wa miaka 44, ameibuka na ushindi wa kihistoria, akiwa ameshinda hata baada ya kuachiwa huru kutoka jela wiki mbili zilizopita.
Ingawa matokeo rasmi bado hayajatangazwa, mpinzani wake, aliyekuwa waziri mkuu na aliyekuwa anaungwa mkono na Rais Macky Sall, amekiri kushindwa.
Rais Sall mwenyewe amempongeza Faye kwa ushindi wake, akimtaja kuwa mshindi.
Ushindi wa Faye unaashiria hali ya kutokua na matumaini miongoni mwa vijana wasio na ajira nchini humo, pamoja na wasiwasi kuhusu uongozi.
Katika hotuba yake ya kwanza kama rais mteule, Faye ameahidi kufungua ukurasa mpya baada ya miezi kadhaa ya machafuko ya kisiasa.

0 Comments:
Post a Comment