Serikali ya Kenya Yazikabidhi Miili ya Wahanga wa Shakahola kwa Familia
Serikali ya Kenya imeanza rasmi kutoa miili ya wahanga wa tukio la Shakahola kwa familia zao.
Zaidi ya familia 30 kutoka maeneo mbalimbali nchini Kenya walikusanyika nje ya Hospitali ya Malindi katika Kaunti ya Kilifi kwa ajili ya kupokea miili ya wapendwa wao iliyohifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti baada ya kufukuliwa msituni Shakahola miezi kadhaa iliyopita.
Stephen Mwiti, ambaye aliwapoteza watoto sita katika tukio hilo, alielezea matumaini yake ya kupokea miili hiyo lakini alikabiliwa na changamoto.
Kero zilizojitokeza zilikuwa ni pamoja na ukosefu wa vifaa na dawa, ambazo zilitajwa na Mwenyekiti wa Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu ya Kenya, Roseline Odede.
Tume hiyo imechukua msimamo wa kutofurahishwa na ucheleweshaji huo na imeelezea malalamiko yake kuhusu jinsi serikali inavyojivuta katika shughuli ya kukabidhi miili kwa familia za waathiriwa.
Awamu ya tano ya kufukua miili zaidi katika msitu wa Shakahola inatarajiwa kuanza tena baada ya miili iliyopo kukabidhiwa kwa familia.


0 Comments:
Post a Comment