Jacob Zuma Apata Ajali ya Gari
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma amehusika katika ajali ya gari lakini hakujeruhiwa.
Ajali hiyo ilitokea Alhamisi jioni, Machi 28,2024 ambapo gari lake rasmi liligongwa na gari lililokuwa likiendeshwa na dereva mlevi.
wakati Polisi wanasema ilikuwa ajali, lakini mwanachama wa chama chake cha uMkhonto we Sizwe (MK) anadai kwamba ilikuwa njama ya kumdhuru.
Zuma, ambaye amesimamishwa kazi na chama chake cha ANC, alikuwa ndani ya gari pamoja na timu yake ya ulinzi wakati wa tukio hilo.
Hakuna aliyejeruhiwa, ikiwa ni pamoja na wanachama wa Huduma za Ulinzi wa Rais.
Rais wa zamani alihamishwa na kupelekwa kwenye makazi yake, kulingana na taarifa fupi ya polisi.
Dereva mlevi mwenye umri wa miaka 51 amekamatwa kwa "kuendesha gari akiwa amelewa na... kuendesha kiholela". Mkuu wa uchaguzi wa chama cha MK, Musa Mkhize, ameonyesha hisia za njama, akisema kwamba walikuwa wakisubiri tukio kama hilo kutokea. Anadai kuwa Rais alionywa kuwa angekuwa katika hatari kabla ya siku ya uchaguzi na kwamba wajumbe wa Kitengo cha Ulinzi wa Rais walifanikiwa kumweka Rais salama.
Zuma, mwenye umri wa miaka 81, alihudumu kama rais kuanzia 2009 hadi 2018, alipolazimika kung'atuka kwa sababu ya tuhuma za ufisadi, ambazo anakanusha.
0 Comments:
Post a Comment