DC ARUSHA ACHARUKA KUPANDA BEI YA SUKARI, WATAKAOUZA ZAIDI YA SH 3000 KUNYANG'ANYWA LESENI



MKUU wa wilaya ya Arusha, Felician Mtahengerwa ametangaza bei elekezi ya sukari kwenye jiji la Arusha kuwa ni shilingi 3,000 ambapo amewataka wanancni watakaouziwa bidhaa hiyo kwa bei tofauti watoe taarifa kwa watendaji wa kata au ofisini kwake ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.
 
Amezitaja hatua hizo kuwa ni pamoja na kuwafutia leseni za biashara na kuwafungulia mashauri ya uhujumu uchumi.


Aidha amempongeza wakala wa sukari ya TPC mkoani Arusha, mkurugenzi wa kampuni ya Alpha Group, Karim Dakik kwa kushirikiana na serikali kuweka mikakati kuhakikisha bidhaa hiyo inawafikia wananchi kwa bei ya shilingi 3,000.

Mtahengerwa ameyasema hayo leo, Januari 20, 2024 wakati alipotembelea ghala la kuhifadhi sukari hiyo akiwa ameambatana  na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya kujionea kiasi cha sukari kilichopo ambapo alikuta tani 307 alizosema zinatosheleza mahitaji ya jiji la Arusha.


Amesema kuwa ana uhakika wa bei aliyotangaza inatekelezeka kwani walifanya majadiliano ya kina na kampuni ya Alpha Group ambayo ni  wakala wa TPC anayesambaza sukari kwenye jiji la Arusha, anawauzia wauzaji wa jumla kwa bei ya shiingi 2,800 kwa kilo hivyo inawezekana kabisa wananchi kuuziwa bidhaa hiyo kwa shilingi 3,000.


Mutahengerwa amewasihi wafanyabiashara wasitumie nafasi hiyo kuwaumiza wananchi kwa kuwapa bei kubwa na watakaokiuka watawanyang'anya leseni ya biashara sanjari na kuwachukilia hatua za kisheria ikiwemo kuwafungulia kesi za uhujumu uchumi.

"Wiki iliyopita niiwaelekeza wafanyabiashara kuuza bei iliyopangwa na serikali ya shilingi 3,000 .Tulitembelea kata zote tukateua wafanyabiashara kadhaa ambao tutawapelekea sukari na gharama ya usafiri sisi serikali ndiyo tutaingia ili kuhakikisha wanauza sukari kwa bei elekezi ya shilingi 3,000," amesisitiza mkuu huyo wa wilaya na kuongeza.


"Wafanyabiashara sitaki kusikia mfanyabiashara yoyote anauza sukari kwa bei ya zaidi ya shilingi 3,000 kwa kilo. Tumeunda kikosi cha kufuatilia wafanyabiashara wanaouza sukari kwa bei ya zaidi ya hiyo watakamatwa na kuwafungulia kesi za uhujumu uchumi,".

Amewaelekeza viongozi wa tarafa na kata kusimamia zoezi hilo, kuhakikisha wananchi wanauziwa sukari kwa bei ya shilingi 3,000 kwa kilo.

"Mwananchi yeyote akiuziwa sukari kwa bei ya zaidi ya shilingi 3,000 akatoe taarifa kwa mtendaji wa kata au aje kwa mkuu wa wilaya mimi mwenyewe nitaenda kwa muuzaji husika na kumchukulia hatua za kisheria," amesisitiza Mtahengerwa.

Aidha ameipongeza kampuni ya Alpha Group kwa uzalendo alioonyesha hasa kwa kuweka mbele maslahi ya wananchi kwa kunakikisha sukari inayoingia Arusha mbali ya kuwauzia wauzaji wa jumla lakini pia anawauzia wananchi mmoja mmoja .


"Sisi kama serikali tunamshukuru na kumpongeza ndugu yetu Alpha Group. kwa sababu kila inapotokea changamoto ya sukari yeye mwenyewe amekuwa mstari wa mbele kutoa ushirikiano, anakuja ofisiji kwetu tujadiliane kuona namna gani sukari iliyopo  itasambazwa kwa wananchi ili wauzwe kwa bei kubwa," amesema Mutahengerwa na kuongeza

 
"Kwa kweli ni wafanyabiashara wachache wenye moyo kama huu. Hapa nchini  tuna wafanyabishashara wengi lakini inapotokea changamoto kama hii huitumia kama fursa ya kuongeza bei ili kujipatia fedha zaidi.

"Dalia ameweka utu mbele sana. Mimi nikuhakikishie kama serikali tutaendelea kukuunga mkono na tutakupa mashirikiano yoyote utakayohitaji kwa sababu ya uungwana wako na namna unavyowajali wananchi


Kwa upande wake, Mkurugenzi wa kampuni ya Alpha Group, Karim Dakik  alisema kuwa yeye anaunga mkono juhudi za serikali kuhakikisha wananchi wanapata sukari kwa bei ya shilingi 3,000 ambapo kwa kushirikiana na maafisa tarafa wamekuwa wakipeleka sukari hiyo kwenye kata mbalimbali za jiji la Arusha.


"Tumeweka matangazo kila sehemu kuonyesha kuwa hapa kwa sasa (kwenye ghals na ofisi zake zilizopo eneo la viwanda  Unga Limitedi)  nawahudumia wananchi wote sukari si lazima iwe kilo 50 . Mtu yeyote anayetaka sukari aje kwangu nitawahudumia," amesema Dalia na kuongeza

"Tumeamua kupeleka sukari kwenye kata ili kuwaondolea wafanyabiashara gharama za usafirishaji jambo litakalowawezesha kuuza sukari kwa bei elekezi na wao wapate faida.



Hata hivyo Dakik amesema kuwa kuna changamoto ya mahesabu kwa sababu kuna maeneo yamezunguka Arusha kama wilaya ya Karatu na mkoa wa Manyara wakikosa sukari huko kwao wanakimbilia hapa kuchukua hivyo kufanya mahitaji ya sukari kuwa makubwa jambo ambalo hata TPC wanalielewa hivyo huwa tayari kuongeza kiwango cha sukari kwa ajili ya Arusha.


Mapema leo Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema hali uzalishaji wa sukari katika viwanda saba nchini imeshuka hadi kufikia tani 1,000 kwa siku kutokana na mvua za El-nino zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini.

Amesema mvua hizo zimeathiri hali ya uvunaji wa miwa mashambani na kupunguza kiwango cha sukari katika miwa kwa zaidi ya asilimia 25.

Akitoa kauli ya serikali leo Jumamosi kuhusu hali ya sukari nchini, Bashe amesema katika kukabiliana na upungufu wa sukari ambao sasa umefikia tani 30,000, serikali imetoa kibali kwa wenye viwanda kuagiza sukari tani 100,000 ambayo inatarajiwa kuwasili nchini tarehe 23 – 24 Januari mwaka huu.

Amesema mahitaji ya sukari kwa siku nchini ni tani 1,500 na kutokana na hali hiyo bei ya sukari imepanda kutoka 2,700, 3000 hadi kufikia 4000.



0 Comments:

Post a Comment