MAHAKAMA imewahukumu kifungo cha miaka 30 jela watu wanne baada ya kukutwa na hatia kwenye kesi ya ugaidi ya kulipua mgahawa wa Traditional Indian Cusine uliopo jijini Arusha.
Aidha imemhukumu Idd Salim Abdallah miaka 18 jela kwa kosa la kuwahifadhi watuhumiwa wa ugaidi.
Uamuzi huo umetolewa faragha leo Desemba 15,2023 na jaji ,Stephen Magoiga aliyesikiliza shauri hilo la jinai (criminal session case) namba 66/2022 ambalo lilianza kusikilizwa kwa faragha Novemba 15, 2023 kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.
Waliohukumiwa miaka 30 jela ni pamoja na Yusuph Ally Hutta, Aman Mussa Pakasi, Rajab Ayub Abdallah na Abashari Hassan Omary ambapo kwa kuwa walikuwa mahabusu miaka tisa hivyo watatumikia kifungo kwa miaka 21.
Awali kwenye shauri hilo kulikuwa na washitakiwa sita waliokuwa wakikabiliwa na mashitaka 17 ya vitendo vya ugaidi ambapo mmoja, Shaban Iddi maarufu kama baba Tuna aliachiwa huru baada ya mahakama kumuona hana kesi ya kujibu,
Washitakiwa hao kila mmoja alikuwa akitetewa na wakili wake akiwemo, Simon Mbwambo, John Shirima, Jabir Wahira
Washitakiwa hao walihusishwa na tukio la mlipuko bomu uliolipuka usiku wa Julai 8,2014 jijini Arusha katika mgahawa wa Traditional Indian Cusine uliopo pembezoni mwa Klabu ya Gymkana ambapo jumla ya watu nane walijeruhiwa.
Tukio hilo lilitokea kati ya saa nne na tano usiku ambapo aliyekuwa kaimu mgamna mkuu wa hospitali ya Seliani Dr. Paulo Kisanga alisema walianza kupokea majeruhi hao kuanzia majira ya saa tano kasoro na saa tano usiku .
Alisema kuwa walipokea wagonjwa nane ambao waliumia sana katika maeneo ya miguu ambapo alibainisha kuwa katika wagonjwa hao nane kuna mmoja ambaye aliletwa akiwa na hali mbaya sana kitu ambacho kiliwalazimu kumfanyia upasuaji usiku huo huo.
"Kati ya wagonjwa hao nane mmoja aliletwa akiwa mahututi sana kwani mguu wake ulikuwa umeadhiriwa sana na bomu hilo ivyo ikatulazimu kumkata mguu mmoja wa kushoto ,kwakweli mgonjwa huyo ambaye tumemkata mguu anaitwa Deepak Gupta (25) mwanaume na sasa hivi anaendelea vyema kidogo na yupo katika chumba cha ICU ndani ya hospitali hii yetu ya Seliani,"alisema Kisanga.
Aliwataja majeruhi hao kwa majina kuwa ni pamoja na Vinod Suvesh(37), Ritwik Khandelval (13), Raj Rajin(30), Prateck Saver, Manci Gupta, (14), Manisha Gupta (36), Mahush Gupta(42) pamoja na Deepak Gupta (25) wote wakiwa na asili ya kiasia
Kisanga alisema kuwa kwa mujibu wa wagonjwa hao walio waliofika hapo hospitali walidai kuwa bomu hilo lilirushwa kwa kupitia dirishani.!
0 Comments:
Post a Comment